Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,664
- 1,228
WAZIRI DKT. NDUMBARO ATEMBELEA MAONESHO TAMASHA LA TAMADUNI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Septemba 22, 2024 amekagua mabanda ya maonesho katika Tamasha la Utamaduni la Tatu la Kitaifa linaoendelea katika Uwanja wa CCM Majimaji Mkoani Ruvuma.
Maonesho hayo yamepambwa na vitu mbalimbali vya Utamaduni ikiwemo vyakula, vinywaji, ngoma na huduma mbalimbali za kijamii.
Aidha, Mhe. Dkt. Ndumbaro amekagua hatua iliyofikiwa katika kilele cha maadhimisho ya Tamasha hilo ambalo litafungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Septemba 23, 2024.
Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro ameambatana na Katibu Mkuu Bw. Gerson Msigwa, Naibu katibu Mkuu Bw. Methusela Ntonda, Wakurugenzi na wakuu wa Taasisi za wizara.