Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameahidi kutoa milioni 5 kwenye harambee iliyoandaliwa na Muhashamu Askofu Flaviani Katindi Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita, kwa kushirikiana na Baba Paroko Padri Japheth Masalu wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome kwa ajili ya ukarabati wa jengo la parokia hiyo.