Waziri Bashe: Nani kasema vijana wa Dar es Salaam hawawezi kulima?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,739
13,503


MBUNGE: UKAGUZI KWA WATUHUMIWA GEREZANI UNADHALILISHA WANAWAKE
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema “Tunawasisitiza RPC, OCD na Wakuu wa Vituo kuzingatia Sheria kwa makosa yanayostahili dhamana, pia Serikali imetenga fedha katika Bajeti ijayo kwa ajili ya kununua vifaa vya kisasa vya kiteknolojia vya ukaguzi.”

Awali, Mbunge Salome Makamba alihoji kuhusu utaratibu wa mtuhumiwa kujidhamini kwa makosa ambayo anaruhusiwa kufanya hivyo kutozingatiwa pamoja na kudai mchakato unaotumika kuwafanyia upekuzi wafungwa na mahabusu hasa Wanawake ni wa kidhalilishaji.

MWITA WAITARA: WANATOA MAJIBU YA UWONGO KUHUSU FIDIA YA MGODI WA NORTH MARA
Mbunge Mwita Waitara amechukua uamuzi wa kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kutoridhishwa na majibu ya Serikali Bungeni kuhusu fidia kwa Wananchi walio karibu na Mgodi wa Barrick North Mara.

Akijibu hoja, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema “Mgodi wa Barrick North Mara ulionesha nia ya kutaka kuchukua baadhi ya maeneo ya vijiji vinavyozunguka mgodi huo, lakini baadhi ya Wananchi wakaamua kuongeza majengo harakaharaka maarufu kama ‘Tegesho’, ndipo mgodi ukaachana na maeneo hayo kwani hayaathiri utendaji wao wa kila siku.”

Waitara akasema “Machi 28, Waziri wa Madini alisema malipo ya fidia yatalipwa kabla ya mwezi wa sita lakini majibu yanayotolewa sasa ni ya kisiasa na yenye maumivu makubwa kwa watu wa Tarime.”


WAZIRI BASHE: NANI KASEMA VIJANA WA DAR ES SALAAM HAWAWEZI KULIMA?
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema “Ni aibu kuhoji kwanini tumemmilikisha Mtanzania ardhi, ni wawekezaji wangapi katika Nchi hii tumewamilikisha ardhi na hawaitumii? Nani kasema vijana walioenda Dar hawawezi kulima? Tumewajaribu wapi? Tatizo tunataka walime kwa teknolojia ya 1960, 70 au 80 hilo haliwezekani.”

Bashe amesema hayo wakati akijibu hoja ya Mbunge, Halima Mdee aliyekosoa utaratibu wa Wizara ya Kilimo kwa kudai anapinga mchakato wa kutafuta Wakulima kama ambavyo wanatafutwa Manesi na Walimu.

 
Back
Top Bottom