Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,092
- 728
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameipokea rasmi timu ya wasichana ya mpira wa miguu ya Fountain Gate, mabingwa wa Afrika kwa Shule za Sekondari walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kimataifa ya mpira wa miguu ya CAF yaliyomalizika hivi karibuni nchini Afrika Kusini.
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewapokea Mabingwa hao leo Aprili 11, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo ameupongeza uongozi wa Fountain Gate chini ya Mkurugenzi Bw. Japhet Makau kwa kuendelea kuthibitisha ubora wa Benchi la Ufundi kwa kufanya maandalizi sahihi ya timu na kupelekea kupata matokeo chanya
"Nakumbuka mara ya mwisho mliniahidi kutwaa ubingwa wa CECAFA tulipokutana Chamazi katika mashindano ya ukanda wetu wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, na kweli mkatwaa ubingwa huo, mara ya pili tulipokutana tarehe 31, Machi 2023 mkaniahidi kutwaa Ubingwa wa Bara zima la Afrika katika mashindano yaliyofanyika Afrika Kusini na kweli mkatekeleza ahadi yenu!" Amesema Mhe.Balozi Pindi Chana.
Amesema kuwa, katika kuendelea kuwapongeza, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, (Mb) ameawalika Bungeni Mabingwa hao Aprili 13, 2023 jijini Dodoma, huku akiongeza kuwa Wizara itatoa zawadi ya Shilingi milioni 10 kwa mabingwa hao.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia amesema zawadi ya Dolla laki 3 waliyopata Mabingwa hao imelekezwa iende katika ujenzi wa Miundombinu ya michezo katika shule hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Shule hiyo Bw. Japhet Makau ameahidi kuendelea kuibua na kuendeleza vipaji vingi kupitia Shule ya Fountain Gate ambao wamekua wanatoka vijana wengi wanaoshiriki katika mashindano mbalimbali ya Mpira wa Miguu kwa wanawake na kufanya vizuri.
Katika Mashindano hayo Timu hiyo pia imefanikiwa kuchukua zawadi ya Mchezaji Bora, Mfungaji Bora na Golikipa Bora.