A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Buswelu, manispaa ya Ilemela mkoa wa Mwanza. Imenibidi nihame nyumba yangu nikapange sababu ya ukosefu wa maji.
Ndani ya wiki maji yanaweza kutoka mara moja tu, ikitokea yametoka mara mbili hyo ni bahati, kuna muda maji yanatoka asubuhi muda wa kwenda kazini na ukirudi unakuta yashakatika.
Wakazi wengi aidha wamehama nyumba zao au wanaogopa kuhamia sababu ya ukosefu wa maji. Gharama za kununua maji kwa wauzaji ni kubwa sana. Mfano mie eneo langu dumu la lita 20 linauzwa kwa mia nne( 400) kwa hiyo muuzaji anauza madumu 5 kwa shilingi elfu 2. Dumu la lita 1000 linauzwa kwa elfu 15. Hizo gharama kwa mtu wa kawaida ni kubwa sana.
Licha ya Jiji la Mwanza na Halmashauri ya manispaa ya Ilemela kuzungukwa na sehemu kubwa ya ziwa Victoria ila upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wengi imekuwa ni changamoto ambayo imekosa ufumbuzi kwa muda mrefu.
Maeneo mengi ya Mwanza yamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji licha ya kujengwa na kumalizika kwa tanki kubwa la maji eneo la Buswelu na pia chanzo cha maji cha Butimba ila usambazaji wa maji umekuwa wa kusuasua.
Maeneo kama Buswelu, Nyasaka, Kahama, Ilalila, Nyamhongolo ndani ya manispaa ya Ilemela na Buhongwa, Mkolani ndani ya jiji la Mwanza maji yamekuwa yanatoka kwa wiki mara moja au mbili na kuna muda hata wiki inapita bila maji kutoka.
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(MWAUWASA) na Wizara ya Maji chini ya Waziri Jumaa Aweso wamekuwa ni watu wa kutoa ahadi za uongo kila siku. Waziri amekuwa ni mtu wa matamko na matukio ila kiuhalisia upatikanaji wa maji maeneo tofauti na mjini ni kero.
Watu wengi wametelekeza nyumba zao tatizo kubwa ni ukosefu wa maji. Sasa najiuliza kama Mwanza yenye chanzo kikubwa na cha uhakika cha maji cha ziwa Victoria hali ipo hivi je tungekuwa tupo kama Singida au Shinyanga hali ingekuaje?
Namshauri Waziri wa Maji na Serikali kwa ujumla kutafutia ufumbuzi hali hii maana ni aibu Mwanza kuwa na tatizo la ukosefu wa maji.