Waziri Aweso: Bwawa la Mindu ni roho ya Wananchi wa Morogoro. Watu kukosa maji wiki 3 Morogoro ni uzembe. MORUWASA Msikae Ofisini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,500
13,119
WAZIRI AWESO AANZA ZIARA YA MOROGORO

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewasili Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuanza ziara yake ya Siku moja ya kukagua na kufuatilia hali ya huduma ya upatikanaji wa Maji katika Mji wa Morogoro

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewataka Wasimamizi na Watendaji wa bonde la Wami - Ruvu kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kuhakikisha mazingira ya Bwawa la Mindu ambalo ni roho ya Wananchi wa Morogoro yanakuwa sawa.

Amesema hayo leo Tarehe 23 Julai 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Morogoro; ambapo anakagua mitambo ya kusukuma maji Tumbaku, kukagua shughuli za uzalishaji maji Mafiga, kushuhudia utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa huduma ya maji - Gairo na kuongea Wananchi

Amesema Bwawa hilo ambalo ni chanzo kikuu cha maji likitetereka litawaweka Wananchi katika mtihani; hivyo ameagiza wahusika kuweka nguvu zaidi katika kulinda na kutunza wa vyanzo vya maji kwa sababu kwenye eneo hilo majani yamesogea mpaka kwenye Bwawa.

Amesisitiza kuwa "hauwezi ukaruhusu majani yamefika mpaka kule na leo tumekuja tumekuta watu wanakata katakata, jambo la pili tumeona makazi ya watu yanazidi kusogea katika chanzo hiki kikuu cha maji, nafikiri tushirikiane sasa, hii sio kazi ya mtu mmoja, na nyie mkubali pia kushirikisha kwa sababu jamii ipo, na Viongozi wapo usipowashirikisha utakwama tu".

Pia, soma: KERO - Waziri Aweso unasema DAWASA kuna hujuma? Njoo Morogoro, huduma ya Maji ni kero kubwa

UPDATE
- Meneja wa usambazaji maji MORUWASA asimamishwa kazi

IMG-20240723-WA0031.jpg
IMG-20240723-WA0045.jpg
IMG-20240723-WA0041.jpg
IMG-20240723-WA0039.jpg
IMG-20240723-WA0064.jpg
IMG-20240723-WA0062.jpg
IMG-20240723-WA0058.jpg
IMG-20240723-WA0054.jpg
IMG-20240723-WA0068.jpg
IMG-20240723-WA0069.jpg
IMG-20240723-WA0066.jpg
 
WAZIRI AWESO AANZA ZIARA YA MOROGORO
View attachment 3049999
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewasili Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuanza ziara yake ya Siku moja ya kukagua na kufuatilia hali ya huduma ya upatikanaji wa Maji katika Mji wa Morogoro

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewataka Wasimamizi na Watendaji wa bonde la Wami - Ruvu kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kuhakikisha mazingira ya Bwawa la Mindu ambalo ni roho ya Wananchi wa Morogoro yanakuwa sawa.

Amesema hayo leo Tarehe 23 Julai 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Morogoro; ambapo anakagua mitambo ya kusukuma maji Tumbaku, kukagua shughuli za uzalishaji maji Mafiga, kushuhudia utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa huduma ya maji - Gairo na kuongea Wananchi

Amesema Bwawa hilo ambalo ni chanzo kikuu cha maji likitetereka litawaweka Wananchi katika mtihani; hivyo ameagiza wahusika kuweka nguvu zaidi katika kulinda na kutunza wa vyanzo vya maji kwa sababu kwenye eneo hilo majani yamesogea mpaka kwenye Bwawa.

Amesisitiza kuwa "hauwezi ukaruhusu majani yamefika mpaka kule na leo tumekuja tumekuta watu wanakata katakata, jambo la pili tumeona makazi ya watu yanazidi kusogea katika chanzo hiki kikuu cha maji, nafikiri tushirikiane sasa, hii sio kazi ya mtu mmoja, na nyie mkubali pia kushirikisha kwa sababu jamii ipo, na Viongozi wapo usipowashirikisha utakwama tu".
Nchi hii inasemekana imepata Uhuru wake kutoka kwa Mkoloni Mwingereza takribani miaka zaidi ya sitini (60) iliyopita, lakini mpaka leo bado tupo tunahangaika kutatua vijitatizo vidogo vidogo kama hivi! How shame it is???
 
Serikali ilifanya uthamini pale ili wananchi waondoke, bwawa litanuliwe, sasa kwa nini hawajalipwa ?

Waziri Aweso aaagize EWURA nchi nzima wawe wanatangaza matokeo ya vipimo vya maji(treatment). Morogoro inasambaza na kukusanya maji taka. Mji umejaa amoeba na taifoid. Ukiongea na waluguru kumi, watatu wana tatizo la kusikia, wanajitutika madozi mpaka ngoma za masikio zinaziba. Regulatory authority asiishie kwenye bei, hata quality ya maji, consumer apate feedback

Mto Mvuha unapita tu na maji yanaenda kumwagwa baharini, kila mwaka Morogoro ina mafuriko.
 
Wanapo ingia ofisini kwanza kwanza wana anzaga kwa kasi sana badae jiiiii kelo zipo pale pale
 
Lukobe Uluguruni ni pipe zimefukiwa chini miaka miwili wanaume wakasepa labda mwakani,mwaka wa uchaguzi watakuja kutulishia matone ya maji ili wapate kura wasepe tena,Daaaaah mambo ni mqgumu jamani
 
Mto Mvuha unapita tu na maji yanaenda kumwagwa baharini, kila mwaka Morogoro ina mafuriko.
Serikali hivi sasa inajenga bwawa la Kidunda, mashariki mwa mkoa wa Morogoro ili kuyazuia na kuyahifadhi maji ya mto Mvuha, Duthumi, Mgeta na Ruvu kwa matumizi.
Kwahiyo ondoa shaka, baada ya ujenzi maji ya mto Mvuha hayataenda tena baharini.
 
Hongera kwa Waziri kwa hizi ziara na kuibua changamoto mbalimbali na kuzipa ufumbuzi. Suala la bill za maji kuwa kubwa kuliko matumizi haswa ukizingatia maji yanatoka mara mbili au moja kwa wiki sio sahihi. Tafadhali litazame hili!
 
Back
Top Bottom