Waziri ataka kiwanda kitaifishwe

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, ameelezea namna mwekezaji wa kiwanda cha Triple S Beef Ltd, asivyo mtu mwema kutokana na vitendo vyake.

Mwijage alisema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (CCM), aliyetaka kujua ni lini Serikali itataifisha kiwanda hicho cha nyama, baada ya mwekezaji huyo kushindwa kukiendesha.

Akijibu swali hilo, Mwijage alisema mwekezaji huyo hata uongozi wa juu wa Serikali unamfuatilia kwa kuwa alitumia kiwanda hicho kuchukua mkopo na hajarudisha.

Alisema kwa sasa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina, wameshakutana na mwekezaji huyo, ambapo walimtaka kuwasilisha mpango mkakati na andiko la mpango wa biashara wa kuendeleza kiwanda hicho.

Mwijage alisema serikali imempa mwekezaji huyo fursa ya kwanza aendeleze kiwanda hicho kama ilivyokubalika katika mkataba wa kuuziana na akishindwa kutumia fursa hiyo, kiwanda hicho kitatwaliwa na wala si kubinafsishwa.

Alimtaka mbunge huyo kutoruhusu hata wananchi kutumia maeneo ya kiwanda hicho, kwa kuwa mwekezaji huyo anaweza kwenda mahakamani na kutumia hali hiyo kama kisingizio kilichomzuia kuwekeza.

Alisisitiza kuwa serikali ina nia ya kurudisha viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi vifanye kazi, viongeze ajira na kuchangia pato la taifa.

Mwijage alisema Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina, inafuatilia mikataba ya viwanda vyote vilivyobinafsishwa na kufanya tathmini ya kina, ili kujiridhisha kabla ya kuvirejesha serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…