Watumishi waliobainika na vyeti feki na kuhisi wameonewa, Waziri Angellah Kairuki amelieleza Bunge kuwa watatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu na nakala kwa baraza la mitihani.
Amesema barua hizo ziambatanishwe na nakala za vyeti vilivyomo kwenye faili lake la ajira na vitapitiwa kwa umakini zaidi.
Ameonya kuwa endapo mtu atakata rufaa wakati anaujua ukweli adhabu itakuwa kubwa zaidi.
Chanzo: Mwananchi