JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,661
- 6,395
Licha ya Serikali kupitia Waziri wa Michezo, Damas Ndumbaro kutangaza kusitishwa kwa Mradi ambao kibao cha ujenzi wake kimeandikwa 'Mama Samia Primary School', Mradi huo umesimama lakini hali ya mazingir bado ipo vilevile.
Kitendo cha Waziri wa Michezo, Damas Ndumbaro kusitisha ni wazi kulikuwa na shida, ili isiwe mchezo endelevu anashauri hatua zichukuliwe lakini tunachojiuliza Waziri alitoa siku tatu tangu Agosti 12, 2024 eneo hilo lirejeshwe katika mazingira ya kawaida ikiwemo kufukia mashimo, hadi leo Agosti 20, 2024 hali bado ipo vilevile.
Pia soma ~ Sakata ujenzi wa Shule kwenye uwanja mpira Panga - Tegeta Wazo kuna harafu ya Rushwa na uzembe, tunaomba TAKUKURU ilimulike