Wazee wetu hawakuwa wajinga kututafutia wake wa kuoa! Wasukuma tulibezwa sana kuhusu hili yamkini waliona mbali.

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
5,827
11,836
Amani iwe nanyi nyote (BabaParoko)

Enzi hizo hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 ilikuwa kawaida kabisa Mzee wa kisukuma kwenda kumtafutia kijana wake binti wa kuoa. Mara zote walikuwa hawakosei mfano ni babu yangu kuwatafutia baba zangu wote wanawake wa kuoa na akalifanikisha wote akiwamo na baba yangu mzazi nae alitafutiwa.

Baba yetu mkubwa nae akachukua kijiti aliwatafutia vijana wake 3 wanawake wa kuoa nae hakukosea (alikufa mapema vijana wake2 wakiwa bado hawajaoa)
Katika hiyo list ya baba zangu na kaka zangu waliotafutiwa wake hakuna hata mmoja ndoa yake ilikuwa na shida kiasi cha kuachana na baba ama kaka zetu hakuna na haijatoea.Kuna baba zangu2 walikufa mapema na mama mmoja alikufa)

Mama zangu ilikuwa kawaida kuachwa mwaka ama na zaidi baba wanaenda kutafuta maisha hasa zanzabar kipindi hicho na wanarudi hata baada ya miaka2 lakini mama zangu walikuwa wanawasubiri bila shida yoyote ile.

Kumbuka kijana wa kileo zama hizo hata simu hamna kwahiyo akiondoka ndo mazima maombi yenu ni kuomba arudi akiwa mzima tu na amepata mali(kukwabha). Mara zote walikuwa wanakuja na treni na hata kwenda pia.....Kumbuka kuwa mara nyingine nyingi walikuwa wanaondoka bila kuaga nyumbani (wake zao) Walikuwa wanaaga kwa babu tu akitoa baraka huyo ametoa akikataa amekataa(wanatii).

Na babu ndo alikuwa anaweza wa kutoa taarifa kwa mama kuwa mmeo kaenda zanzibar kutafuta hapo ni baada hata mwezi ama zaidi na anaweza kuja kwa kukuambia ameota zaidi 3 ndoto inajirudia rudia ileile kuwa magadula yupo zenji kumbe aliagwa.

Turudi kwnye mada sasa.Kwanini wazee wa kisukuma walikuwa na wajibu wa kwenda kuwatafutia vijana wao wake wa kuoa?
Wazee wetu walikuwa watafiti na wadadis sana kwenye maswala nyeti kama haya.Ikumbukwe kuwa hata kijana alikuwa hakatazwi kabisa kuchagua mke amtakaye hapana alikuwa anaruhusiwa vizuri tu.

Wewe kijana ukimpata huyo binti kabla ya mambo yoyote yale lazima ulete taarifa kwa mzee wako na kisha mzee ataenda kuchunguza upya na ikiwa ataridhia basi utajitwalia mke huyo kama huyo binti hafai utaambiwa huyu hapana na iwapo utashupaza shingo basi mzee anaweza asihusike kwenye mahali au atakubali sawa lakini watakuja kushindwana kwenye mahali


Hizi ndio sifa kuu walikuwa wanaangalia wazee wetu.

MAGONJWA;Hili lilipewa kipaumbele sana sina haja ya kuelezea wengi wenu hadi leo hamuoi kwa ma albino nk japo wazee walikuwa wanaangalia vitu vingi hasa magonjwa ya kurithi nk.

TABIA;Kama familia hiyo mnatabia za wizi hata kama kuna wanawake wazuri kiasi gani ilikuwa ngumu mno kuolewa.Tabia nyingi mbovu lilikuwa ni doa kubwa mno.

UCHAWI/USHRIKINA;Ni kigezo kingine kilikuwa kinaangaliwa sana kwa jicho la tatu na hata kwenda kwa sangoma kuchek maabara kwanza.

FAMILIA HIYO INAISHI NA WATU BAKI?;Wala usiulize hii ilikuwa na umuhimu wake ukumbuke zamani umimi haukuwepo.Ni kigezo kilichokuwa kinaangaliwa pia hii ni kwa sababu walijua fika kama binti kakua kwenye familia ya kaka na dada bila na watoto wa mjomba na watu wa kuja ni ngumu sana kuweza kuishi na watu wengine ambao familia yenu inaishi nao kama wanafamilia.

USIMBA NA YANGA WA KIPINDI HICHO; Huku kulikuwa na ngoma za asili(utamaduni)hizo ngoma zilikuwa zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni WAGIKA NA BHAGALO.Mfano rahisi ni kwa sasa tungesema ni simba na yanga.Ilikuwa ni marufuku kipindi hicho kuoa kwa wagika kama wewe ni ni mgalu(bhagulo wingi mgalo umoja) siyo kuoa tu hata kuazima kitu kama chumvi jembe nk ilikuwa marufuku.Hivyo walikuwa wanaoana wao kwa wao tu yaani simba anamuoa simba mwenzake na yanga hivyo hivyo.Hii walikuwa wanatuhumiana kuwa upande huu ni wezi na wengine ni wachawi nk nk.

RANGI YA MWANAMKE;Hiki sio kigezo kikubwa sana kama ilivyokuzwa na watani zetu wazaramo,wagogo,warugulu nk kuwa wasukuma wanapenda wanawake weupe hapo msukuma atatoa ng'ombe hata 100 wazaramo acheni wivu wenu mbona ninyi mnamwaga radhi mchana kweupe hatujawahi wasema popote?

Ukweli ni kwamba mwanamke mweupe anapendwa karibia na wanaume wengi sana na hii imepelekea dada zetu wa ki Africa kujikoboa na kuwa weupe.Leo hii wanawake weusi ni kati ya viumbe waliombioni kutoweka duniani.

Kwa wasukuma ni tofauti kidogo kilichokuwa kina angaliwa ni kwamba ni sawa wewe ni mweupe je! tabia za wazazi wako,familia yako na wewe mwenyewe ni njema ama la? Iwapo tabia zako ama zote kwa ujumla ni mbaya hakika hakuna mwenye kujitambua atakuoa na weupe wako.Na iwapo tabia zitakuwa nzuri hakika utapewa mang'ombe mengi sana.Hii dada yangu alipewa ng'ombe 37 wa kujichagulia zizini.

TABIA ZA MAMA YAKE NA BINTI;Haijarishi familia ina ukwasi binti ni mzuri na ni bikra Baba yake binti anatabia njema nk lakina kama mama wa mji huo ni mchawi,roho mbaya,hana nidhamu kwa mme wake nk basi mji hiyo ilikuwa ni ya kuogopwa!!


vigezo vingine tutaja kwenye comment uzi usiwe mrefu sana.

Leo hii vijana mmepewa uhuru wenu mnajitafutia wake ninyi wenyewe na wazazi wenu wanakuwa wanahusika ama kwa 10% tu Maana unakuta kijana mahali umetoa mwenyewe nk wazazi wana husika kwenye keki tu.

Swali ni je kwanini ndoa zenu za kujitafutia wenyewe hazidumu kuliko za wale waliokuwa wanatafutiwa?

Unatoa wapi uhali wa kuwacheka wale walio tafutiwa wake na bado wanaishi vyema tofauti na ndoa zenu za mwendo kasi?


Vijana wenzangu nimewahi waambia hapa kuwa hakuna jambo jepesi kwa mwanaume kama kutafuta mke wa kuoa hakuna! Unaweza maliza mwaka mzima hujapata kabisa.Hii hutanielwa hata niseme nikiwa uchi wa mnyama pale post ama kariakoo sana sana mtaniona chizi tu.

Ni wakumbushe ukiamua kuoa hata kesho tu unaweza kujizolea ukaweka ndani lakini huko ndani kukawa hakukariki kabisa ndio ninyi mnaleta uzi hapa kila siku mmeyatimba hakika ukichunguza lazima kuna mahali ulifeli ndio maana mnageuka washauri ghafla....... mnatia huruma sana.

Iko hivi mimi kipindi nahitaji kuoa nilikuwa na mahusiano na mabinti kadhaa(3) hawa ni serious relation.Lakini nilipowaweka kwenye matazamio kwanza wote3 hawakuwa mabikira! kitu ambacho hadi babu anakufa alikuwa ananimbia akishalewa kuwa usioe mke wa mtu kisha anarudia babuuuuu usioe mwanamke asie bikra!!

Achana na babu ambaye ni mwanaume bibi kizaa mama alikuwa anasema vilevile kuwa usioe mwanamke asie bikira anatoa na sababu nzito sana.


Kwahiyo hao watatu walikoswa vigezo sio kuwa bikra na issue zingine kadhaa wa kadhaa mmoja wapo alikuwa amejitoa ufahamu sana kwangu akawa ananiibia hadi vitu kwao siku moja akaiba kwao akamkuta bro alipoondoka Bro akasema huyu ukioa atakuwa anakuiba tena anapeleka kwao!.........Kumbuka nilienda hadi kwenye makambi ya wasabato nikaambulia kipingo tu na nikatoka bilabila .....fuatilia kuna uzi humu unasema JINSI NILIVYO AMBULIA KIPIGO KWENYE MAKAMBI YA WASABATO.

Baada ya kufanya jitihada zangu zote na kugonga mwamba nili surrender kwa mzee wangu nikamwambia mzee fanya kama alivyokufanyia babu asee. Mzee hakugoma aliitikia na kuingia mzigoni japo nae alifeli.Kwa sababu sasa nilikuwa nimedhamilia kuoa na ili niweze kufanya biashara yangu lazima niwe na mwanamke nilienda kwa dada yangu ambae anaweza akanizaa pasina shaka maana watoto wake2 wananizidi umri kutoa wasiwasi kuhusu sisi tumezaliwa zaidi ya12!


Dada ni mkatoriki safii kabisa amedumu kwenye uongozi sana na ana watoto wengi sana mabinti wa kiroho (ubatizo) Nikamwelezea A-Z akasema hilo limeisha kabisa labda kama unataka mwenye sifa zingine kama makalio mrembo sana nk.


Dada akaingia mzigoni siku3 tu nikaambiwa njoo uone ukiridhia sawa ...sikwenda kazi zilinibana kama baada ya wiki nikaongea na shem mme dada aingie mzigoni nae kumdadisi yule binti shem akakubali akasema nipe wiki2 Imagine binti kapatiakana ndani ya siku3 tu lakini shemeji kumchunguza akasema nimpe wiki2 wewe kuweza?

Nikakubali......Shem namuamini na nilijua dada anaweza niangusha ila shem hawezi yeye sasa ni mkubwa pengine wanaweza zidiana miaka kama 10 tu na mzee asee.

Shem alikuwa hamujui yule binti kabisa hivyo hakupaswa amuulize dada zaidi ya kumwambia nasikia shemej anataka kuoa kwa flani huyo binti anaitwa nani? jina akapewa na kwenda kufanya kazi.

Shem akafatilia hadi akampata alipomuona mwonekano wa nje akasema anafaa,akaanza ku dili na marafiki zake na huyo binti akajiridhisha, akadiri na wazazi wake bahati nzuri wanafahamiana walikuwa wanajuana vyema hasa huko kanisani, Shem akafanya ujasusi mwingine wa kuwatumia vijana wa kitaa kujua kuwa huyu demu ni wanani na kashaliwa na nani?

Vijana wakaleta jibu pasina shaka kuwa demu huyu ana mahusiano ya na kijana muuza duka ila kaambiwa kula mzigo hadi ndoa. Maneno haya kasema kijana mwenyewe na hawezi danganya mama lake letu. Tofauti na hapo hapa mtaani huyu binti hana mwanaume mwingine....

Nikiwa sijui hili wala lile na wazo la kuoa kama linataka kutoka tena by saa6 mchana shemeji akanipigia akasema njoo uchumbie binti yupo safi unaweza kuendelea na dada yako sasa mimi nimemaliza na usimuache huyu binti ni wachache sana wa hivi.Muda huo huo nikaongea dada,dada akasema nilikuwa nimeona labda umepuuzia maana ulikaa kimyaa karibia wiku3 zote enhee niambia unakuja lini? mimi jtano.

Elewa hili hadi naenda sijawahi ongea na binti kwa njia yoyote ile kipindi tunafika kwa dada mi nilikuwa na jamaa yangu ikapigwa simu kwenye mji huo kuwa saa9 mna wageni ....aliyekuwa amepenyezewa hizi taarifa ni mama wa binti tu kuwa kaka yangu anahitaji awe mkwilima wenu.



Muda ukafika tukaenda hapo kumbuka sijawahi muona binti wala yeye kuniona hata wazazi wake tu sijawahi waona.

Inshort tulichumbia tukakubaliwa na ndoa ikafungwa siku ya siku binti alikuwa bikira na sijawahi juta hadi leo hii. Matatizo madogo yenyewe yapo tu .

NB: SIYO LAZIMA UTUMIE NJIA YANGU. Nikisa changu mimi ili uone kuwa hakuna mwanamke wa kuokota barabarani na kumuita mke hakuna lazima ujute tu kama sio leo basi kesho.

Kwakweli nimemaliza kama uzi umekukera kwa urefuuu nisamehe sipendelei kuishia njiani halfu niseme itaendelea sipendelei.

Manyanza SHIMBA NGOSHA S @Shimba ya Buyenze
 
Back
Top Bottom