Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 338
- 704
Ulaghai wa mahusiano mtandaoni hutokea pale ambapo mtu anaamini yuko kwenye mahusiano na mtu mwingine 'tapeli' katika Mitandao ya kutafuta wachumba 'dating sites' kama vile Tinder na OkCupid
DALILI ZA ULAGHAI WA MAHUSIANO MTANDAONI 'CATFISHING'
JINSI YA KUWA SALAMA 'DATING SITES'
DALILI ZA ULAGHAI WA MAHUSIANO MTANDAONI 'CATFISHING'
- Tapeli hujaribu kwa nguvu kukushawishi kuwasiliana naye nje ya mtandao mliokutana, kama vile kwa barua pepe au simu.
- Tapeli anauliza maswali mengi kukuhusu ili kupata taarifa zako binafsi.
- Mara nyingi huepuka mawasiliano ya ‘video’ au kukutana ana kwa ana.
- Hutumia picha za kuvutia ili kushawishi. Unaweza kutumia ‘Google Reverse Image Search’ ili kujua wapi picha hizo zimetumika kabla.
- Hakuna taarifa zao [Tapeli] kwenye mitandao mingine ya kijamii.
- Baada ya muda wa uhusiano [Mapenzi au Urafiki], wanatafuta sababu za kukuomba pesa au utapeli wa aina nyingine
JINSI YA KUWA SALAMA 'DATING SITES'
- Iwapo wewe ni mtumiaji wa Mitandao hii kumbuka kulinda taarifa zako binafsi kwenye mitandao hiyo, tumia Mitandao ya Mahusiano inayoaminika kupitia 'App Store' na 'Google Store'. Pia epuka kuwasiliana nje ya Mitandao hiyo kwa sababu wanaosimamia mitandao hiyo ni rahisi kuwatambua tapeli
- Aidha utakapokuwa na wasiwasi wa mhusika ulikutana nae katika mitandao hiyo kumbuka kufanya utafiti wa taarifa zake katika mitandao mingine, Hakikisha mnawasiliana kupitia 'Video call' ili kuhakikisha unaenda kukutana na mtu sahihi. Na endapo mtafanya mpango wa kukutana kumbuka kutoa taarifa kwa ndugu na marafiki kuhakikisha usalama wako. Iwapo utagundua dalili za ulaghai usisite kuripoti kwa wahusika wa mitandao hiyo