Pre GE2025 Wazee mashuhuri mkoa wa Tabora Wafanya Matembezi Kumpongeza Viongozi wa CCM kwa Kuteuliwa Kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
644
1,444
Viongozi wa dini, wazee mashuhuri pamoja na wakazi wa mkoa wa Tabora, wamefanya matembezi katika kila kona ya manispaa ya Tabora kwa lengo la kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuteuliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa kuwania kiti cha Urais kwa mwaka 2025.

Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa matembezi hayo, wameeleza sababu za kumpongeza Rais huku wakiomba serikali kuweka wagombea pia katika ngazi za chini ambao watawaletea maendeleo.

Soma Pia:

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhandisi Deusdedith Katwale wamesema wataendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuimarisha maeneo ya kihistoria mkoani humo.

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Ally Nkumba, ameeleza sababu za kuchagua wagombea wao mapema katika nafasi mbalimbali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
 
Njaa haijawahi kumuacha mtu bila wenge
 
Back
Top Bottom