NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,573
- 13,408
Kumekuwa na makelele ya vijana wakisema ndoa ni wizi, utapeli na kupotezeana muda nk.
Ndoa za sasa ni tofauti kabisa na ndoa za zamani, mama na baba zetu walidumu kwenye ndoa kwa muda mrefu bila kutokea fujo/mvunjiko wakuachana labda itokee mambo ya kibinadamu tu, kama vikombe kabatini vinagongana sembuse binadamu wasipishane kauli? Hapana lazima itatokea tu lakini ndoa zilidumu tofauti na sasa.
NALIA NGWENA nataka nizungumze mambo makuu mawili yaliyowafanya wazee wetu wadumu katika ndoa zao tofauti na vijana wa sasa(vijana wa hovyo) wasiotaka kusikia neno ndoa.
(1) Wazee walipangiwa mke/mume wakuoa au kuolewa naye, hii ilisaidia sana maana unapokwenda kuoa unakuta wazee wako wanaujua vizuri ukoo huo.
Kama wana magonjwa ya kurithi, washirikina, wavivu wa kulima nk, kutokana na wazee/mababu kujua ukoo fulani ulisaidia sana, wazee wetu waliambiwa wakaoe kwenye koo nzuri zenye tabia njema, chapa kazi nk.
(2) Jando na unyago, baba zetu na mama zetu walipewa elimu namna gani yakuwa mvumilivu unapokuwa kwenye ndoa, mambo ya ndani yabaki ndani.
Jando hii hutumika kwa watoto wa kiume kukaa kambi/porini pale wanapokuwa wamefanyiwa twahara, wanapokua kambi wanapewa mafunzo na wazee namna gani ya kuishi katika ndoa na maisha kwa ujumla.
Unyago/kukaa mwali haswa kwa mabinti waliovunja ungo kukaa ndani kwa muda wa miezi kadhaa huku akipewa mafunzo ya ndoa na mtu maalumu anayeitwa kungwi. Hii iliwasaidia sana mama zetu kujua namna gani yakuwa na nidhamu kwa mume wake na ilipelekea wadumu kwenye ndoa.
NALIA NGWENA haya machache nimeyapata kwa babu yangu mwamba kabisa mzee Ngwena, kaamua kunimegea machache haya.
Ni kweli kizazi cha sasa kinaendeshwa na globalization (utandawazi), unakutana na binti mjini hujui hata robo ya background yake unaweka ndani anaanza kukusumbua kumbe genetically ndivyo alivyo.
Wife materials wapo wengi/wakutosha vijana tutulize vichwa tuoe lakini siyo kukaza shingo na kuanza kulaumu wanawake wote.