Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,983
- 65,144
Hahahaha!
Nimeona niwasalimu kwa kicheko.
Miaka kadhaa iliyopita, ndugu zangu ambao baadhi Yao ni wananafasi za uongozi huko CCM walikuwa wakichukizwa Sana na Tabia yangu ambayo kwao waliona haina Tija.
Mara kwa mara walikuwa wakinishinikiza niwe upande wa CCM kama wao walivyo.
Robert huko unapotea,
Robert hao ni matapeli
Robert umelogwa na Nani, yaani akili zako zote unashindwa kuuona UKWELI.
Robert njoo huku, utafika mbali huko unapoteza Muda.
Mimi sipo CHADEMA, Hilo ndilo jibu langu sikuzote.
Hauko CHADEMA wakati siku zote wewe unakuwa upande wao. Na unaoonekana umfuasi wa Lissu.
Nawajibu, ninyi waonevu Sana.
Basi wakanizoea hivyohivyo.
Sasa jana nipo Kanisani, ndugu yangu Mmoja hivi Kada wa CCM ni kama alikuwa anataka IBADA iishe tuonane. IBADA kuisha akaniwahi kabla sijaondoka.
Akanisalimu huku akatabasamu; Vipi mwanamageuzi?
Nikabaki nimetabasamu.
Akaniambia; Mjomba sikukuu hizi tuimalizie huku CCM. Acha ubishi wako. Kila kitu kiko wazi.
Ikaja Uber nikamuacha hapo ananitania.
🥴🥴 Ndani ya Uber nimemaindi mchango. Ananitumia meseji. Ikiwa inasema.
Watibeli hawatumikii vibaraka daima.
Hawatumikii vibaraka wa miungu Wala wa mashetani.
Ni aidha wamtumikie shetani mwenyewe au Mungu MWENYEWE. Siku Njema Mjomba.
Nikazima simu.
Robert Heriel
Mtibeli
Mlimani City, Dar es salaam