Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,920
- 50,274
Kutokana na jua kuwa kali, ardhi kuwa kame, na mazao kukaukia shambani; baadhi ya wazazi wamekuwa chachu ya kuwashawishi mabinti zao waingie kwenye mahusiano biashara. Yaani mdada anaingia kwenye mahusiano ili apate kitu, hasa hela; ili aweze kuwahudumia wazazi wake.
Mabinti wamegeuzwa kuwa vitega uchumi wa familia, na mwanaume atakayejichanganya kwenye hayo mahusiano, atachunwa mpaka afilisike; na pesa ukiishiwa, unakimbiwa.
Wakati mwingine, wazazi wanawashawishi mabinti zao, wahakikishe wanaporudi nyumbani waje na kitu ili maisha yasogee.
Kama mwanaume, ni vizuri kushtuka mapema na kuchukua hatua.