Mwana umleavyo ndivyo akuavyo.
Sikatai mtoto mpende utakavyo, lakini jiulize na kesho yake itakuwaje? Kweli mtoto wa kidato cha kwanza hajui kufua, kupika?
Daah! Gari la shule linaharibika hajui namna ya kufika nyumbani? Wazazi hii ni sawa? Mtoto kila anapokwenda anapelekwa na dereva, hajui kupanda daladala?
Hii ni sawa hii. Mtoto wa namna hii unategemea ataishi vipi kama haupo? (Mungu aepushie mbali) au kama shekeli zikikata je?
N>B.
Sina maana mtu umchukie mwanao, La hasha...Lakini mlee katika njia inayofaa ili aweze kuyamudu mazingira yamzungukayo au vinginevyo.
Mtoto kudharau watu masikini, mtoto kudharau watu ambao si wasomi ni kwamba anajijengea ukuta. Mara nyingi watoto wa namna hii future yao huwa mitihani.
MZAZI AMKA, MLEE MWANAO KATIKA NJIA IMPASAYO.
TAFAKARI!