Wazazi boresheni lishe kwa watoto, wengi ni wafupi kuliko wastani...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
Tulikuwa mahala tunaangalia mashujaa wetu wa mpira wa miguu umri chini ya miaka 17 dhidi ya Mali Kuna vitu tumejikuta tunatafakari.

Pamoja na kiwango kikubwa walichoonyesha kupambana na mabingwa hao watetezi na kutoka suluhu watoto wetu walionekana wenye maumbile madogo madogo sana ukilinganisha na mahasimu wao wenye umri Sawa.

Kuna tafiti kadhaa zimefanyika na kuhitimisha kuwa watoto wetu wengi wana kimo kilichochini ya wastani.
changamoto hii iwaendee wazazi na wote wanaotarajia kuwa na watoto kwamba ni afadhali mzazi ulale njaa kuliko mtoto kukosa mlo kamili kipindi anapouhitaji zaidi. Ikishindikana basi tujitahidi watoto wapate kikombe cha maziwa kwa siku.
 
Kuna issue ya genetics za mtu, kama mtu ni mfupi haijalishi atakula nini atabakia hivyo hivyo.

Lakini pia ukweli usiopingika ni kwamba watanzania wengi wamedumaa.
Kweli mkuu
Kuna watu wengine wanaamini ni wafupi kwa sababu wamerithi kumbe tatizo ni lishe
 
Kuna ukweli aisei..! Ingawa Tanzania mwaka jana ilippat namba moja Africa kwa watoto wenye afya bora.
Taasisi ya bill and merinda gate iliwahi kutafiti na kusema watoto wetu wengi wenye miaka 13 wanaurefu wa wastani wa mtoto mwenye umri wa miaka Saba. Wakashauri wasiache kunywa maziwa ktk umri huo....
 
Kwa mfano Baba Ni mfupi na mama Ni mfupi halafu mnategemea mtazaa watoto watefu? Hata kama watoto mtawalisha balanced diet ya namna gani hawawezi kurefuka.
 
Kwa mfano Baba Ni mfupi na mama Ni mfupi halafu mnategemea mtazaa watoto watefu? Hata kama watoto mtawalisha balanced diet ya namna gani hawawezi kurefuka.
Inawezekana kama tatizo la ufupi wa hao wazazi sio genetics Bali wote Kila mmoja kwa nafasi yake walidumaa utotoni
 
Kweli mkuu, umasikini nyumbani hasa tuliokulia uswahilini ni tatizo. Kinachpoatikana mzazi akileta mambo ya balance diet mtaishia kufirisika. Ila ni kujitahidi kadili inavyowezeka
Swala la kipato nalo linachangia
 
Muanzisha uzi, tangu lini Pituitary Gland ikachochewa na vyakula? Au darasa la 6 sikumuelewa vizuri mwalimu wangu!?
 
Kwa mfano Baba Ni mfupi na mama Ni mfupi halafu mnategemea mtazaa watoto watefu? Hata kama watoto mtawalisha balanced diet ya namna gani hawawezi kurefuka.
je kama hao wazazi na wenyewe walikosa kupata/kwa kutokujua virutubisho ambavyo vingeweza kuchochea ukuaji/urefu...cha msingi ni kuzingatia lishe bora tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…