Wawili wafariki, mmoja apooza kwa mstuko wa bomoabomoa

Ngida1

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
586
206
Wawili wafariki, mmoja apooza kwa mshtuko wa bomoabomoa

Watu wawili, Moris Thomas na Kobero Peter wamefariki dunia na mwanamke mjane mwenye watoto 10, Mwashamu Hassan amepooza ikidaiwa kuwa ni baada ya nyumba zao kuwekewa alama X. Wote ni wakazi wa Mtaa wa Kigogo, Mbuyuni, Kinondoni.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu iliyopita na ilidaiwa kuwa marehemu hao na mama huyo walipatwa na mshtuko ghafla kuanguka.

Kobero alipoteza maisha papohapo na Moris alipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu ambako alikaa kwa siku moja lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuhamishiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Muhimbili ambako alifariki dunia Jumanne asubuhi.

Mjane apooza
Akisimulia mkasa huo juzi akiwa amekaa kwenye kipande cha godoro nyumbani kwake, Mwashamu alisema baada ya kuona nyumba yake ikipigwa X, alipatwa na mshtuko na kupooza ghafla kuanzia kiunoni hadi miguuni na kwamba hawezi kutembea tena.

Alisema amekuwa akiishi katika nyumba hiyo aliyoijenga na marehemu mumewe Omary Hassan kwa miaka 15 sasa.

“Hii nyumba nimeijenga na mume wangu kwa kudunduliza pesa, nikiuza karanga yeye akifanya vibarua.Tumeijenga kwa Sh12 milioni,” alisema.

Alisema alikuwa akiishi kwa kutegemea nyumba hiyo yenye vyumba sita vya wapangaji na viwili alivyokuwa akiishi na watoto wake.

“Kila mwezi nilikuwa napokea Sh30,000 kwa kila chumba kutoka kwa wapangaji, sikuwa anapokea kodi ya miezi sita wala mwaka,” alisema.

Mmoja wa watoto wa mama huyo, Ibrahimu Hassan alisema ilikuwa saa 3.35 asubuhi wakati wanakunywa chai waliposhangaa kuona kundi la watu wakiwamo askari wenye bunduki waliokuwa na chupa ambazo walikuwa wakizipuliza ukutani na kuandika neno “Bomoa”.

“Tulibaki kushangaa hatujui nini kinaendelea, tuliuliza kuna tatizo gani tukaambiwa tunatakiwa kubomoa nyumba zetu, baada ya kusikia hivyo mama alianza kulalamika anajisikia vibaya,” alisema Hassan; “ilibidi tumnyanyue kumuingiza ndani ili asione kinachoendelea, tukashangaa kufika jioni mama hawezi kusimama wala kutembea.”

Hassan alisema kabla ya hali hiyo mama yao alikuwa anafanya kazi ndogondogo licha ya kuteguka mgongo kutokana na ajali na kuwekewa vyuma ambako alipewa masharti na madaktari ya kutofanya kazi nzito wala kupata mshtuko wa aina yoyote.

“Tayari mama ameshapata tatizo, hapa unavyoona tangu tukio hilo litokee hawezi kutembea, wapangaji wote wamehama, wengine walitakiwa kutulipa kodi tarehe 13 mwezi huu lakini haiwezekani,” alisema.

Hassan alisema kutokana na hali ngumu ya maisha yeye na ndugu zake hawana kipato cha kumsaidia mama yao.

“Wengi wetu tumeishia darasa la saba, tunafanya vibarua vidogo kumsaidia mama kupata pesa ya kula na kusomesha wadogo wetu,” alisema.

Majirani
Majirani wa mama huyo wamemlilia Rais John Magufuli wakitaka awaonee huruma wananchi wake akiwamo mjane huyo ambaye sasa amepata maradhi yaliyosababishwa na bomoabomoa.

“Magufuli ulisema unampenda Mungu na unawapenda watu maskini,” alisema Saumu Mohamed huku Juma Mkude akisema: “Kama hivyo unavyomuona ni mama wa watoto 10, wengine bado ni wadogo watakwenda wapi?”

Mjumbe wa nyumba kumi, Maya Hatibu alisema: “Hali yake kama unavyomuona, hawezi kutembea tena mwenyewe alikuwa anafanya vijikazi vidogovidogo vilivyokuwa vikimwingizia kipato cha kila siku.”

Nyumbani kwa Moris
Akizungumza katika ibada ya kuaga mwili wa Moris iliyofanyika nyumbani kwake Kigogo Mbuyuni kabla ya kusafirishwa kwenda Kijiji cha Matombo, Morogoro alikozaliwa, kaka wa marehemu, Colneus Thomas alisema mdogo wake alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu na siku walipofika kuweka alama X alikuwa amekaa nje.

Alisema marehemu ameacha mke na watoto watatu na kwamba nyumba hiyo ilikuwa ya urithi wa baba yao na familia yao ilikuwa ikiishi hapo tangu mwaka 1970.

Mtaa wa Mburahati – Barafu
Kazi ya kuweka alama X katika nyumba 1,934 lilikuwa ikiendelea katika Mtaa wa Mburahati – Barafu jana na wakazi wa eneo hilo walionekana kupigwa butwaa huku wakisema “Tunajuta kwa nini tumemchagua Magufuli.”

Jana, Abdallah Bulembo aliyekuwa meneja wa kampeni wa Rais John Magufuli alilishutumu Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akisema: “NEMC wasiwe kama wameshuka kutoka mbinguni na kukuta watu wamejenga mabondeni. Wasituharibie imani ya wananchi kwa Rais.”

Pia, baadhi ya wananchi walijikuta wakiimba nyimbo za CCM: “Acha waisome nambaeeee...CCM mbele kwa mbele.”

Mama mjane, Janeth Kunambi aliketi chini na kuanza kuangua kilio baada ya nyumba yake kupigwa X. “Nitakwenda wapi sasa... nina watoto wanataka kwenda shule, nawaza wataendaje leo mnaniongezea zigo jingine nani atanitua?”

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Bonaventure Baya alisema katika mtaa huo nyumba 1,934 zimewekea alama X na watu wote wanatakiwa kuondoka kwa hiari yao.


Chanzo: Mwananchi
 
Last edited:
Haya tena, tushaanza kumuhesabia mzee. Wawili hao washakuenda na mmoja huyo yupo njiani!
Tutaisoma namba mwaka huu!
 
Mi naamini kidhati kabisa hii nchi imejaa MATIKITI MAJI WENGI NA SIYO BINADAMU TUNAWADHANIA SISI,inakuwaje we mtu timamu ufurahie wenzio kuvunjiwa nyumba kisa ujione kuwa ulikuwa sahihi kuichagua ccm!!!?jijue ubongo wako haujatimia so jitafakari upya ndugu,hayajakukuta na yaliyowakuta waliropoka kama wewe na sasa wanajuta,KOSA NI LA SERIKALI NA SI LA WANANCHI,serikali ndiyo inayopaswa kuandaa mazingira ya wananchi kujenga na kukataza maeneo yanayofaa na yasiyofaa kabla wananchi hawajajenga,JIULIZE WATU WANGAPI WANA HATI ZA NYUMBA HAPA NCHINI!!?JE NI VIWANJA VINGAPI VIMEPIMWA!!!?JE IWEJE WATU WAZALIANE HAPO NA KUZEEKEA HAPO NA LEO WAAMBIWE WAMEJENGA PASIPOFAA IKIWA SERIKALI IPO SIKU ZOTE!!!?IWEJE VIWANJA HAVIJAPIMWA MPK LEO IKIWA WANANCHI WANAONGEZEKA KILA KUKICHA NA KUHIITAJI ARDHI YA KUJENGA!!!?THINK TWICE
 
AISEE INAUZUNISHA SANA,,LAKINI NA IMANI MUNGU ATAWALIPIA IKO SIKU DHIDI YA HII DHURUMA ,,,SEHEMU ZINGINE WAMEVUNJA HAMNA HT RECORD KWAMBA PALIWAI KUKUMBWA NA MAFURIKO,,, ,,,,,HALAFU UNAKUTA JITU LINAFURAHIA MTANZANIA MWENZIE KUVUNJIWA NYUMBA
 
Inahuzumisha,tuliwaambia huyu mtu amekuwa katili kwa mkewe anayelala nae sembuse kigagula?

Wewe Sunzu ni ya ukweli haya uyasemayo au umo kwenye utani tu? Kwanini basi msitueleze siku zile za kampeni? Doooooooo tumekula hasara basi. Ikiwa ni katili kwa mkewe sidhani kama ataonesha huruma kwa mwananchi mwengine yoyote yule. Huyo mkewe kwani anamfanyia ukatili gani???
Anyway, ndio twaisoma namba sasa!
 
AISEE INAUZUNISHA SANA,,LAKINI NA IMANI MUNGU ATAWALIPIA IKO SIKU DHIDI YA HII DHURUMA ,,,SEHEMU ZINGINE WAMEVUNJA HAMNA HT RECORD KWAMBA PALIWAI KUKUMBWA NA MAFURIKO,,, ,,,,,HALAFU UNAKUTA JITU LINAFURAHIA MTANZANIA MWENZIE KUVUNJIWA NYUMBA

Please, usihadithie. Unatuengeza uchungu. Hata huyo mkoloni asingetufanyia kama hivi. Leo ni wenyewe kwa wenyewe tunafanyiana maovu kama haya. Mtu imemchukuwa miaka 30 kuijenga nyumba yake, leo ghafla hanayo tena au anapewa kiwanja, atakifanya nini? Tusije kustaajabu wakatokea katika hawa waliovunjiwa nyumba zao wakajiunga na ISIS!
 
Wala sio ya uwongo hayo uyasemayo kaka/dada yangu.
Yan cjui hawa wana mioyo gan???? mjane unamvunjia nyumba hujamwonyesha pa kwenda na watt kumi!! Mungu anasisitiza kwe habar dini kuwa"DINI SAFI NA ISIYOKUA NA MAWAA NI KWENDA KUWATIZAMA WAJANE NA YATIMA KTK HALI ZAO.
 
mtu ukitafakari sana unaweza unahuzunika mwenyewe tu, wakoloni tunawalaumu ila walijenga mashule ambayo mpaka hiv karibuni walivoleta shule za kata shule nying za zaman ni zao, reli mpaka leo hatujawahi kuongeza chochote zaidi ya maneno tu, japokuwa walikuwa wakatili lkin sehem nyingi walizokaa kuna plan na mipango inayoeleweka mfano south, hawa waswahili wanaotwambia tuko huru yan ni sawa bure kabisa, viwanja hawapimi yan miaka 50 ya uhuru nchi nzima imepimwa chin ya asilimia 30, wakipima wanagawiana wenyewe, unakuta mmoja anavyo kumi, sie masikin tumeokoteza vihela vyetu, tukijenga kiholela walivyo washenzi wanasubiri mpaka tumalize wanakuja kubomoa, hiv mtu akisema bora wakoloni anakosea kweli?
 
mimi nikikumbuka ile siku ya jamaa kutangazwa mshindi, jirani yangu aliweka sauti kubwa sana kua wacha waisome namba eeee, kimpango wao, naniliu mbele kwa mbelee.
 
Inahuzumisha,tuliwaambia huyu mtu amekuwa katili kwa mkewe anayelala nae sembuse kigagula?
Hivi wangesombwa na Maji kama ambavyo imekuwa ikitokea ungekuja na nyimbo gani?

Mmeng'ang'ana na dar tu utadhani mna maisha ya mazuri! Njooni huku mikoani muone tulivonawiri kwa maisha na makazi bora!

Endeleeni kudanganya watu kwa kujipa kazi za Madaktari! Eti wamepooza kwa sababu ya bomoa, JINGA NYIE
 
Mungu uwaponye waathirika wa utekelezaji huu.

RIP marehemu wote.

Serikali fanyeni cost benefit analysis mnapotekeleza majukumu yenu.
 

Makoja, wala sijui kama unafahamu tunakizungumzia kitu gani hapa. Kuwaondoa kutoka mabonde ya maji sio jambo baya, ni jambo zuri sana. Hakuna mwenye akili timamu anaelaumu hilo. Tunalaumu kwamba the whole process haikuwa planned vizuri, imefanywa kiwendawazimu wazimu tu na watu kufurahia shida za wenziwao. Huwezi kumvunjia mtu nyumba na ukamwambia ninakusaidia usikumbwe na maji na ukamwacha alale kwenye mitaro ya maji taka.
Mimi wala sipo Dar, nipo Timbirinzi, Pemba huku, lakini ni lazima nipate huruma juu ya hao ndugu zetu wanaoteswa na serikali yetu wenyewe. Unataka kuwahamisha watu ni lazima ujue watakuenda wapi. Wameachwa na serikali wajenge na leo wanahamishwa na kutupwa nje, hivyo ni jambo zuri kweli hilo?
Leo wameona haya na ati wanasema wenye viwanja vya serikali watashughulikiwa. This is too late and too little!
Sisi watu weusi hatuna mipango hata kidogo. Na wala tusijisifie kwa kufanya jambo zuri au la maana lolote lile, kwani baada ya siku mbili tatu tutatoa uharo hapo hapo kama huu wa sasa. Ni juzi tu tunasifia vita dhidi ya rushwa na leo tunauwana wenyewe kwa wenyewe, tayari ndugu zetu wawili washapoteza maisha na mmoja kapooza kwa balaa lililofanya kwa makusudi.
Unampa mtu kiwanja na kumueleza akajenge, atajengea nini? Hata kufikiria uwezo wa maisha ya watu wa chini upo vipi hatuwezi, kwasababu sisi tupo juu? Babu yangu alisema zamani kuwa "sisi watu weusi ni chakula cha simba tu"!
 
Kwa nini hawakubomoa awamu ya JK???

Sio wameona kuwa huyu bwana Magufuli anaenda vizuri kuipiga vita rushwa?
Kwahivyo, nae anapigwa vita chini kwa chini. Hayo maelezo ya serikali yaliyotolewa are NOT convincing at all. Hawapo kuwasaidia watu. Ni shaghalabaghala tu. Wa hali ya chini wataendelea kubomolewa na watajijua wapi watahamia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…