Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 258
Takriban wavuvi 115 wanatibiwa katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, baada ya kutoka baharini wakiwa na vidonda vya maumivu kwenye ngozi.
"Sio ugonjwa wa kuambukiza - haiwezekani", anasema Karamba Kaba, daktari katika Hospitali ya Donka, akiongeza:
"Tulisoma kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna 'ugonjwa wa ajabu ambao umetokea' lakini watu wanahitaji kuhakikishiwa. Tuna uhakika kuwa wameathirika na kemikali, nikimaanisha kuwa si kuugua kwa kumgusa mtu mwingine."
Hospitali zinatoa huduma ya afya bila malipo kwa yeyote anayekuja na majeraha haya. Matibabu huanza na uchunguzi wa damu na sampuli zinachambuliwa katika maabara za Conakry. Vidonda vya wagonjwa pia huwekwa dawa ili kuwawezesha kupona.
Baadhi ya watu wamekuwa na vidonda usoni, wengine tumboni au sehemu za siri na kuna hofu kwamba baadhi ya wagonjwa wanaogopa kujitokeza kwa ajili ya matibabu.
Kulingana na daktari anayeishi katika kisiwa kilicho kilomita 50 kutoka Conakry, wavuvi wengine saba wagonjwa walienda kwenye kituo cha huduma ya afya cha kisiwa hicho lakini walikataa kwenda katika kituo cha huduma maalum huko Conakry kwa ajili ya kupata matibabu.
CHANZO: BBC