Wavuvi waiomba Serikali kuingilia kati suala la uvuvi haramu kwenye mabwawa ya Kindai na Singidani

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536

Mvuvi katika bwawa la Kindai manispaa ya Singida, Mzee Salumu Kikomeko (84),akionyesha moja ya vyandarua vya mbu vinavyotumiwa na wavuvi haramu katika bwawa hilo. Matumizi ya vyandarua katika uvuvi ni kinyume na sheria za uvuvi.


Mvuvi katika bwawa la Kindai mjini Sngida, Salumu Kikomeko (84), akionyesha samaki aliowavua jana katika bwawa hilo. Kikomeko ambaye amevua katika bwawa hilo kwa miaka 58, anasema uvuvi kwa sasa umeathiriwa na matumizi ya nyavu haramu pamoja na vyandarua vya mbu.
Na Nathaniel Limu, Singida
Baadhi ya wavuvi wanaofanyia shughuli zao katika mabwawa ya Kindai na Singidani manispaa ya Singida, wameilalamikia halmashauri ya manispaa hiyo kwa kutelekeza mabwawa hayo,kitendo kinachochangia wavuvi kutumia nyavu haramu na vyandarua vya mbu ambazo zina athari kubwa kwa ustawi wa samaki.
Wamedai nyavu haramu pamoja na vyandarua vya mbu zinazotumika kwa miaka mingi kwenye mabwawa hayo,lakini manispaa ya Singida imekaa kimya bila kuchukua hatua zo zote za kukomesha uvuvi huo haramu.
Wavuvi hao wamemwomba Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Mh. Mwigulu Nchemba kuja Singida mjini kutumbua jipu hilo,ili rasilimali hizo za mabwawa iweze kusaidia kukuza uchumi wa manispaa na wa wakazi wake.
Wakizungumza na Mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, wavuvi hao wamedai kwamba manispaa ya Singida, imeyapa kisogo mabwawa hayo ambayo kama yangetunzwa vizuri, yangetoa ajira kwa wakazi wengi.
Wamedai kuwa kwa miaka mingi sasa mabwawa hayo yamekuwa kama hayana mwenyewe, kwa sababu kilimo na ujenzi wa nyumba unafanyika kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria kwa shughuli za kibinadamu.
“Hivi sasa sheria ya kulinda rasilimali hiyo ya mabwawa,hazifuatwi.Baadhi ya watu wanalima na kujenga nyumba kwenye maeneo ya mabwawa hayo na kusababisha maji kukauka kwa kasi kubwa na kupunguza vina vya maji.Kisheria shughuli za kibinadamu zinapaswa kufanywa zaidi ya kilometa 60 kutoka kwenye chanzo cha maji”,alifafanua Salumu Kikomeko (84) ambaye amevua samaki katika mabwawa hayo kwa kipindi cha miaka 58 sasa.
Kikomeko alisema amejitahidi mara nyingi kumwomba Mkurugenzi wa manispaa ya Singida wakutane, ili aweze kumpa ushauri utakaowezesha manispaa hiyo kunufaika zaidi na mabawa hayo,lakini juhudi hizo bado hazijazaa matunda.
“Mabwawa haya katika miaka ya nyuma,yamesaidia watu wengi kujiendeleza kiuchumi,kujenga nyumba na kugharamia masomo ya watoto wao.Baada ya kutelekezwa na mamlaka husika,sasa nyavu haramu,vyandarua vya mbu na shughuli za kibinadamu zinafanyika bila shida”,alisema.
Akifafanua zaidi,Mzee Kikomeko alisema zamani mabwawa haya yalikuwa yanafungwa kwa shughuli za uvuvi kwa kipindi cha miezi sita, ili kutoa fursa ya samaki kuzaliana na kuongezeka,lakini sasa kwa muda mrefu utamaduni huo umeachwa.
Naye Juma Kidimanda,alisema wakati umefika sasa kwa manispaa ya Singida kuzinduka na kutambua kuwa mwenyezi Mungu ametoa rasimali ya mabwawa hayo ilindwe na kutunzwa, ili iweze kunufaisha kizazi cha sasa na kile kijacho.
Samsoni Salalii alisema baadhi ya wavuvi wanavua kwenye mabwawa hayo baada ya kukosa kazi za kuwaingizia kipato cha kuhudumia familia zao,na badala yake wamejiingiza katika uvuvi haramu.
Kwa upande wake Afisa uvuvi halmashauri ya manispaa ya Singida, Dk.Kahemela,alisema wameunda vikundi vya wavuvi kwa lengo la kulinda na kuwakamata wavuvi haramu katika mabwawa hayo.
“Katika ofisi yangu tupo wachache na wavuvi wanavua samaki mchana kutwa na usiku pia,kwa hiyo inatuwia vigumu kuwadhibiti wavuvi haramu. Majukumu ya kudhibiti uvuvi haramu, tumeviachia vikundi hivyo”,alisema.
Aidha, alisema wakati wowote wataanza kukagua mabwawa hayo na vyanzo vya maji,watu watakaobainika wanalima au wamejenga nyumba ndani ya kilometa 60,watawajibika kwa mujibu wa sheria ikiwemo nyumba zao kuvunjwa.
 
Jipu hili linazidi kukua!
Yaani hata hapa Dar Ikulu kilomita hata kumi hazifiki watu wana vua samaki kwa mabomu?

Haya ni madharau dhidi ya wanausalama au na wao ni majipu?
Naamini hapa Kazi tu kitaeleweka! Kwa taarifa uvuvi wa Mabomu siku maji ya bahari yakitulia ni siku salama kwa uvuvi wa Nyavu na Mabomu!


cc Paw Moderator
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…