Wauzaji wakubwa wachache

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
650
OLIGOPOLY


Characteristics-of-Oligopoly.jpg

Kwanza neno oligopoly limetoka kwenye maneno mawili ya ki latin maana yake ni wauzaji wachache.

Sifa za Oligopoly:
1.Ugumu wa kuingia kwenye hili soko

Kutokana na mtaji wake kuwa mkubwa, vibali kuwa vingi nk

Mfano:

Biashara ya usafiri wa ndege, mtaji wake ni mkubwa, vibali na masharti nayo ni mengi hivyo ni ngumu kuanzisha hii biashara.

2. Wanategemeana na kushirikiana.
Wauzaji wa hili soko wanategemeana na kushirikiana endapo ataingia muuzaji mpya na kuamua kushusha bei zaidi, basi wao watashusha bei zaidi yake ili muuzaji mpya akose wateja.

Muuzaji mpya akishakosa wateja basi itamlazimu kufunga biashara, akifunga biashara wao watapandisha bei na kuendelea kula faida.

Mfano:

Makampuni ya simu yalivyoshirikiana kwenye swala la tozo za serikali Tanzania.

Wote wakapandisha gharama za kutoa pesa kwenye mitandao ya simu.

3. Matangazo.
Kwenye hili soko ni lazima kampuni iweke pesa kwaajili ya kujitangaza, ukishindwa kujitangaza basi utajikuta makampuni mengine yanakushinda.

Mfano:

Ving'amuzi Tanzania, Kila ukitembea maeneo ya Dar es Salaam basi lazima utakutana na matangazo ya tamthilia zinazoonyeshwa kwenye king'amuzi flani, ukisikiliza radio pia wanatangaza bei za ving'amuzi na offer zake.

DSTV wana tangaza kila siku bei zao, offer zao nk

Startimes pia hawapo mbali katika kujitangaza.

Azam nae kila siku anajitahidi kutangaza king'amuzi chake.

4. Bidhaa zinaendana.

Zote zina matumizi sawa lakini kuna utofauti kutokana na branding.

Example:

Wauzaji wa simu:

Kuna iPhone, Sumsung, Huawei,Vivo,Nokia, Oppo,Techno nk

Hizo ndio moja wapo ya sifa kuu za oligopoly.

Karibuni kutoa mifano ya biashara ambazo zipo kwenye hili kundi la oligopoly.

#oligopoly #biashara #swahili #uchumi
 
Back
Top Bottom