Wauza unga waja na mbinu mpya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Wafanyabiashara haramu ya dawa za kulevya nchini wamebuni mbinu mpya za kukwepa kukamatwa na vyombo vya usalama wanapofanya biashara zao.

Kwasasa wanasafirisha dawa za kulevya kwa kuzichomekwa kwenye nepi za kutupa (pampers) na taulo za kike (pads).

“Ni vigumu kushtukia mzigo unapokuwa umewekwa vizuri kwenye pedi au pampers na kufungwa upya. Tumekuwa tukifanya hivi na hakuna mtu anayeweza kudhani kama tumebeba unga,” anasema mmoja wa watu wanaofanya biashara hiyo wakati akimfunda mwenzake eneo la Kinondoni mwishoni mwa wiki.

Inaelezwa kuwa wamelazimika kutumia njia hiyo ambayo ni vigumu kubaini uwepo wa unga katikati yake ukiwekwa.

“Katika pedi kuna dawa ambayo huwekwa kuitunza. Tunapofumua tunahakikisha karatasi ya juu ya nailoni hatuigusi zaidi ni kuchomoa pamba ya katikati na kuweka unga uliofungwa vizuri kuuchomeka eneo ilikotolewa pamba, kisha tunachukua gundi maalum na kurudishia eneo lililokuwa na pamba,” anasema binti mrembo bila kufahamu kuwa mdukuzi wa habari hizi anamsikiliza.

Anasema wanavyopakia unga kwa kutumia njia mpya si rahisi kukamatwa au kubainika katika mashine za ukaguzi zinazotumika kukagua mizigo katika viwanja vya ndege nchini.

Anaeleza kuwa baada ya kufungwa vizuri, hulazimika kuhakiki usalama wa mzigo kwa kuupitisha katika mashine maalumu kabla ya kuusafirisha.

Mashine imekuwa ikitumiwa kuhakiki usalama wa mzigo (unga) uliofungashwa kitaalam usibainike katika nchi husika na kurahisisha usafirishwaji wake.

“Kabla mzigo haujasafirishwa unafungwa vizuri na kupitishwa kwenye mashine hiyo ili kuhakiki usalama wake. Iwapo kutakuwa na shaka ya kubainika kwake, basi unafunguliwa na kufungwa upya na kuupitisha tena kwenye mashine. Ukishaonyesha kuwa uko sawa ndipo unaposafirishwa,” anamwambia mwenzake.

Imeelezwa kuwa kutokana na ufungashaji madhubuti wa dawa za kulevya na kuhakikiwa na mashine, ni vigumu kuzibaini kutokana na utaalam unaotumika.

“Ukweli ni vigumu kutambua kilichomo ndani ya huo mzigo baada ya kuufunga na kuupitisha kwenye mashine, hivyo mashine hiyo inarahisisha kusafirisha mzigo bila kuwa na shaka ya kukamatwa kama hapo awali,” Anatamba.

Pia imeelezwa kuwa katika ufungaji wanatumia karatasi za kurudufisha (carbon papers)ambazo husaidia kuficha kilichomo ndani ya mzigo.

“Ipo mizigo inayofungwa kwa kutumia carbon papers ambazo ni vigumu kubainisha kilichomo ndani, ingawa mingine hunyunyiziwa marashi maalumu ambayo mbwa wanaotumiwa kunusa hawawezi kubaini lolote,” anasema Dada mrembo wakiwa katika salon ya kike wakirembeshana nywele.

Akizungumza na JAMHURI, Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, ACP Mihayo Msikhela amesema kwani imekuwa mara ya kwanza kusikia mbinu hizo kutumika nchini.

Anasema anachofahamu ni kwamba mbinu hizo zimekuwa zikitumiwa nje ya Tanzania, lakini si jambo la ajabu kuona zimeanza kutumika nchini.

Amesema kinachohitajika ni umakini wa askari waliopo katika mashine za mizigo kwa viwanja vya ndege.

“Nimesoma kupitia mitandao kuwa nchi za wenzetu wameanza kutumia mbinu hizo, lakini jambo la muhimu ni umakini wa askari walio kwenye mashine za ukaguzi. Kwa hapa nchini bado hatujamkamata mtu yeyote anayetumia njia hii mpya, ila mashine zetu za ukaguzi ziko vizuri sana,” anasema Kamanda Mihayo.

Anabainisha kuwa changamoto kubwa iliyopo katika kukabiliana na usafirishaji wa dawa za kulevya ni mipaka ya nchi kuwa wazi na kutokuwa na mbwa wa kutosha wanaoweza kubaini dawa hizo.

Kuhusu wauza unga kumiliki mashine za kukagua mizigo, amesema wafanyabiashara hao haramu wanaweza kumiliki hizo mashine kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kifedha na njia wanazobuni kukwepa mikono ya dola.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Hamad Masauni hakutaka kuzungumzia suala hili kwa maelezo kuwa yuko kwenye kikao hata baada ya kutafutwa kwa zaidi ya wiki mbili ofisini kwake na kuachiwa ujumbe wa maandishi

Wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kurahisisha usafirishaji wa ‘unga’ ambapo mwaka 2012 walikuwa wakiwatumia wanawake wajawazito kusafirisha dawa hizo bila kukamatwa.

Wajawazito walisafirisha ‘unga’ bila kukamatwa kutokana na mashine za ukaguzi kushindwa kutambua dawa za kulevya zaidi ya kuonyesha kiumbe kilichopo tumboni kwa mwanamke husika.

Walifanikiwa kuwatumia wajawazito kutokana na kutoruhusiwa kupita katika mashine mara kwa mara wakaanza kuwashawishi mabinti kushika mimba kwa ajili ya kusafirisha dawa hizo.

Pamoja na kutumia wanawake wajawazito, pia walibuni mbinu ya kutumia mabarafu na sigara.

Kumekuwa na idadi kubwa ya Watanzania wanaokamatwa na dawa za kulevya ambao wapo katika magereza mbalimbali nje ya nchi.

Taarifa zinaonyesha kuwa Watanzania 176 wanatumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini China, huku asilimia 99 wakiwa wamekamatwa kwa dawa za kulevya.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini, zinaonyesha kuwa Watanzania 103 wamekamatwa nchini Brazil kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, huku wengine 132 wakikamatwa katika nchi nyingine, ikiwamo Pakistan.

Pia wafanyabiashara hao wameelezwa kutumia fukwe za baadhi ya hoteli kubwa za kitalii jijini Dar es Salaam kuingiza dawa za kulevya nchini.

Waharifu wamekuwa wakitumia fukwe hizo kutokana na kutotiliwa shaka na vyombo vya dola hivyo kuwa rahisi kuingiza ‘unga’ bila kubughudhiwa.

“Ni vigumu kushtukia mambo yanayofanywa katika fukwe ambazo zipo katika hoteli za kitalii. Huko wamekuwa wakiingiza mizigo ya ajabu ajabu huku vyombo vya dola vikiwa havijui lolote,” anasema mmoja wa watu waliohojiwa ambaye ni mfanyakazi wa moja ya hoteli za kitalii jijini Dar es Salaam.

Mizigo mingi, haramu na halali husafirishwa kwa kutumia boti ambazo hutia nanga karibu na hoteli na kushusha mzigo bila kushtukiwa.

“Mfano mzuri ni hotel ya (jina linahifadhiwa). Hoteli hii imekuwa kichochoro cha bidhaa hatari nchini. Watu wanafanya yao bila kujali kuwa kuna dola Unga umekuwa unapita kila mara. Ndiyo njia yao kuu, lakini hakuna mtu anayeshtukia hata.

“Ukifika pale ufukweni ukakaa tu, utaweza kuona watu wanakuja na boti yao, wanashusha mzigo halafu kuna watu wanakuwa wamekaa hotelini wanawasubiri. Wakishafika wanachukua mifuko yao na kuweka katika mifuko na kuondoka tena kwa kupita hapo hapo hotelini Hii ni hatari kwa usalama wa nchi na hoteli husika,” anasema.

Taarifa zinaonyesha kuwa hivi sasa wahalifu wamekuwa na mazoea ya kutumia fukwe bila hofu yoyote jambo ambalo si la kawaida.

Source:Jamhuri
 
Tatizo mamlaka zetu zimelala sana tafuta na jinsi lady pepeta zinavyotumika ndio ujue wajomba wamejipanga
 
Hii biashara haiji kuisha kamwe.

Na tunachokosea ni pale yakikamatwa na kutaja thamani eti '.. madawa ya kulevya yenye thamani ya bilioni 10 yakamatwa..' hapa ndio wanatutia tamaa ya kuingia kwenye hii biashara.

BTW hivi yule Bint wa Amatus Liyumba alitoka?
 
Sijaskia hyo habar,atakua bado Lindi
 
hivi kwanini kinondoni kunanuka kwa biashara ya madawa ya kulevya?
 
Sorry ....kama kuna mtu ana-contact na hao wauzaji,naomba anisaidie nipige Pesa, ntakupa zawadi .....
 
Mumeanza kunivutia kuifanya hii biashara. Inaonekana inalipa sana. VP natakiwa kuwa na mtaji wa kiasi gani kama beginner wa biashara hii? Je,kwa hapa bongo niwatafute kina nani ili wanipe uzoefu wa kuifanya hii biashara? Kwani hakuna kiongozi wa serikal ambaye anafanya hii biashara ili nijiunge nae tufanye biashara? Billion 10 sio mchezo jaman. Msaada wenu pls
 
HIYO KITU INAFANYWA NA WATAALAM WA PACKING....KUNA PACKING AINA NYINGI KUNA
PACKING UNGA UNA WEKWA KWENYE MASHATI MAPYA...YAANI KILA SHATI WANAWEKA MFUKO MMOJA...
KUNA PACKING ZA KWENYE VYOMBO VYA NDANI YAANI VIKOMBE,SAHANI ETC
IPO YA KWENYE VIATU SEMA NOW DAYS ISHASHTUKIWA...IPO PACKING ZA KWENYE MISHUMAA N'A VINYAGOO....
DUNIANI AU KTK MABEACH YA UNGAA WA PERU N'A WABOLIVIA NI MAMASTER KTK PACKING.....
KUNA MABORDER MENGINE UKIPITA HADI MTOTO WAKO ANAPIGWA SACHI...

OVA
 
hivi kwanini kinondoni kunanuka kwa biashara ya madawa ya kulevya?
Kinondoni ndiyo wasafiri wa kwanza ktk miaka ya 89-90 ambapo mabaharia ndy walikuwa watu wa kwanza kuingiza unga tz wengi wao walikuwa wanaishi kino....ila wakati Huo unga ulikuwa hautumiki....unga ulikuwa unapitishwa TU iko kwenda ulaya,Kabla ya unga ulikuwa madrax ndy deal..
Unga ulipoanza tumika TU ndy watu wakaanza kufata india...india kukawa kugumu wakahamia Pakistan....Pakistan kukawa kugumu....wakahamia iran....kote huko unga ulikuwa unafatwa n'a watu walikuwa wanaumeza mzgo ili kuleta huku...
Ila kwa sasa unga unakjaa kwa majahazi......n'a maboti yani ton n'a maton yanaletwa..

Ova
 
Duhh
 
Mbinu mpya
 
Jamaa ni wabunifi sana. Hawalali wanajitahidi kuvumbua mbinu za kusafirisha madawa kila uchwao!!
 
Biashara ambayo wakati wowote unaweza kuuwawa na wenzako au vyombo vya Dola.

Watakatishaji wakubwa wa pesa duniani na wana uwezo wa kumweka Rais madarakani ktk mataifa ambayo biashara hii imeshamiri.

Watoto waliozaliwa na wakina mama watumiaji...addicted na watoto hao walianza kutumia madawa hao wakiwa ndani ya matumbo ya mama zao kiasi cha kuzaliwa wakiwa wategemezi tayari wa madawa.

Kiwango cha maambiki ya virusi vya ukimwi na homa ya ini viko juu sana kwa watumia madawa kuliko jamii ya kawaida.
 
Hao waangalie makala za Airport Security NatGeo waone wenzao Colombia wanavobaini kwa kutumia sniffing dogs na maabara wanazo palepale mobile laboratories, wanaweka unga kwenye reactant na kubaini ni aina gani mtuhumiwa anapigwa pini hapohapo na kuwekwa!,Ndaani!...Sio mpaka eti tupeleke SAMPULI kwa mkemia mkuu wa sirikali akhah!,mnaenda huku nyuma wanapita saba...Nunueni maabara zile mobile na muwe na sniffing dogs wanaojua sampuli zote za drugs mtafanikiwa kiasi...vinginevyo dooh!

Hizo mbinu nyingi zinafahamika ila
1.Wanaficha kwenye soli ya viatu
2.Wanaficha kwenye sakafu ya begi
3.Wanaficha kwenye circuit board ndani ya diode na capacitors
4.Wanaficha kwenye K..u..m...æ na wengine wana ingest kwenye intestines
5.Wanaficha kwenye parcels zinazotumwa kwa couriers wakiamini hizo hazichunguzwi sana
6.Wanaficha kwenye kucha bandia
7.Wanaficha kwenye laptops na hand gadgets of the like kv simu janja
8.Wanaficha kwenye kwenye Sovenils vijizawadi kama toys etc
9.Wanaficha kwenye cosmetics
10.Wanawatumia V.I.P wakiwemo political, religions na Business people kuvusha wanajua pahala kama hapa kwetu baadhi yao hawakaguliwi sana.
11. Wanaficha kwenye ndege hususani private jets
nk hii biashara anaijua lucifer jinsi alivoipangilia na kuiasisi maana ni ngumu kuimaliza...ila kazaneni
 
"Wajawazito walisafirisha unga bila kukamatwa kutokana na mashine za ukaguzi kushindwa kutambua dawa za kulevya zaidi ya kuonyesha kiumbe kilichopo tumboni kwa mwanamke husika "

Hayo maneno ni ya kamanda ? Hivi kwani kwenye viwanja vya ndege huwa watu wanakuwa scanned au mizigo ndiyo inayopita kwenye X-Rays mashine ?

Huyo mtoto anaonekana vipi wakati watu wanapita kwenye walk through metal detectors na sio X- Rays machine?

Ile mionzi haitakiwi kupita kwenye mwili wa binadamu ndio maana mashine kama Rapiscan au Astrophysics zina plastic nyeusi kuzuia mionzi kutoka nje ya mashine

Haya ni maajabu ya Tanzania au sijui mimi ndio nipo outdated
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…