tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,318
- 4,613
Andiko hili limechochewa na habari ya kujinyonga kwa mwanajeshi William Chacha Giriago huko Dodoma, na malalamiko ya wastaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania ambayo yako kila siku, kuhusu wao kukosa Bima ya Afya.
JWTZ linajinyumbulisha kuwa lina hospitali pande zote, kuweza kutoa huduma kwa watumishi wao, hivyo kwao kuwa na Bima ya Afya si muhimu. Halafu kuna tishio la kiusalama.
Ukweli, ukiacha Lugalo, vituo vyao vya afya ni duni sana. Vina wataalamu wachache wenye sifa, pia vinapungukiwa na vifaa tiba.
Ikiwa waajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania, watajiunga na Bima ya Afya, hapa ifanyayo vizuri ni NHIF, itawapa uhuru wa kutibiwa hospitali yeyote nchini Tanzania inayotoa huduma hizo. Kuwapa unafuu watumishi walioko kazini kutibu wategemezi wao kama baba na mama kwa kuwakatia bima za wategemezi ambao huwa hawapati huduma za hospitali ya jeshi bure.
Kupunguza gharama za bajeti ya matibabu zinazotengwa kwa ajili ya jeshi kila mwaka gharama ambazo zinaweza zikatumika katika maeneo mengine ndani ya jeshi (tetesi zinasema hili fungu ni moja ya sababu inayowafanya wakubwa kule jeshini wasiruhusu jeshi kujiunga na NHIF, maana hili ni fungu tamu).
Jeshi likijiunga na NHIF, hospitali ziendelee kupokea kadi za NHIF, ila uchakataji wa madai yao upewe dawati maalumu, kama lile la NHIF za TISS.
Wastaafu wengi wa NHIF wanateseka mitaani kwa kukosa matibabu bora. Hii ni hatari. Wanajeshi walioko kazini wanapata sonono ya kutibu familia zao (zilizo mbali na maeneo ya jeshi), katika hospitali bora zilizo karibu na wategemezi, na pia wanahangaika kutoa pesa za matibabu kwa wazazi wao, kwa sababu hawana Bima ya Afya, ambayo ingetibu na tegemezi.
Angalia wastaafu wa TISS, Polisi, Magereza na Uhamiaji wanavyotesa kwa kutumia kadi zao za Bima.
Serikali ilitazame hili kwa jicho makini.