Watumishi MOI zaidi ya 1000 wapewa zawadi kuchochea hamasa ya kuwahudumia wagonjwa

informer 06

Member
May 11, 2024
57
42
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetoa zawadi za Sikukuu ya Krismas kwa watumishi wake 1052, ikiwa lengo kuwaongezea motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wagonjwa .

Miongoni mwa zawadi hizo ni Kilo 15 za mchele, lita 2 za mafuta ya kupikia na vinywaji zenye thamani ya Tsh. 50,000 ambazo zimekabidhiwa leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kwa wawakilishi wa watumishi hao na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI, Balozi. Dkt. Mpoki Ulisubisya ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuiongoza taasisi hiyo.
IMG_9923.jpeg

Akikabidhi zawadi hizo Dkt. Mpoki amesema kuwa menejimenti ya MOI imewapa motisha watumishi wake ya mkono wa Sikukuu ya Krismas kwa kutambua mchango wao mkubwa wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.

"Menejimenti ya MOI tumetoa zawadi na shukurani hizi ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wenu mkubwa hususani wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa, pia tunaomba msheherekee sikukuu kwa amani na furaha"- amesema Dkt. Mpoki

Kwa niaba ya wenzake Mhudumu wa Afya wa MOI, Amina Makunga ameishukuru menejimenti ya MOI kwa kuwapatia zawadi hizo, ambazo amesema kwamba zitakuwa chachu ya hamasa na motisha ya kufanya kazi zaidi ya kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.
IMG_9922.jpeg

Ikumbukwe kwa maelezo ya hivi karibuni yaliyotolewa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Lemeri Mchome ni kwamba wagonjwa wanaolazwa kwenye taasisi hiyo kwa siku ni zaidi ya 350.

Akizungumza katika Kikao cha Tano cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa MOI, alisema kwamba wanatarajia kuanza kuhudumia wagonjwa wa nje 1,500 hadi 3,000 kwa siku.

Hatua hiyo ni baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa mitatu ya ujenzi wa jengo jipya ya Wagonjwa wa Nje (OPD), kukarabati jengo la Hospitali ya Tumaini na ujenzi wa Kituo cha Utengamao Mbweni.
IMG_9921.jpeg
 
Kilo 15 za mchele,
lita 2 za mafuta ya kupikia na
vinywaji zenye thamani ya Tsh. 50,000
 
mitandao ya simu siku hizi hata mb za sikukuu hawatoi
 
Wangewapa tu Gift Vouchers. Kila mtu akajibebee anachotaka kulingana na mahitaji yake.
 
Kg 15 2000 =30,000
Mafuta kg 2 @6,000
Vinywaji =50,000

At minimum, kila mmoja alizawadiwa vitu vyenye thamani ya 86,000.

Watumishi 1,052

Zawadi ya motisha inalamba 90,472,000.

Ila mgonjwa akifa na deni la Million 3, maiti haiondoki.

Astagafirullah!.
 
Kg 15 2000 =30,000
Mafuta kg 2 @6,000
Vinywaji =50,000

At minimum, kila mmoja alizawadiwa vitu vyenye thamani ya 86,000.

Watumishi 1,052

Zawadi ya motisha inalamba 90,472,000.

Ila mgonjwa akifa na deni la Million 3, maiti haiondoki.

Astagafirullah!.
Acha wapewe kosa moja haliwezi wakosesha wafanyakazi wote, wanafanyakazi jamani
 
Back
Top Bottom