covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 6,579
- 16,379
Niliposikia kuhusu tabia za Baltasar Ebang Engonga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (ANIF) la Guinea ya Ikweta, alinikumbusha rafiki yangu wa chuo. Rafiki huyu alikuwa na tabia zinazofanana sana na huyu Engonga, hasa katika masuala ya wanawake.
Nakumbuka nilipokuwa mwaka wa kwanza chuo, tulikutana na huyu jamaa na tukawa marafiki wakubwa. Tabia zetu zilifanana kiasi, ila yeye alinizidi kwa kiwango kisichokuwa na mipaka. Katika semesta ya kwanza, tayari alikuwa ametoka kimapenzi na wasichana zaidi ya 14 wa chuoni. Kufikia semesta ya pili, alianza kuhamia hadi vyuo jirani, na kufikia jumla ya wasichana 25 aliofanikiwa kuwa nao kwa mwaka wa kwanza.
Mambo yalizidi zaidi alipofanikiwa kuwa kiongozi kwenye serikali ya wanafunzi kama waziri wa loans chuoni. Katika mwaka wa pili, semesta zote mbili, alitembea na wasichana 75 na wamama watatu. Alipofika mwaka wa tatu, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Kilichonisikitisha ni jinsi alivyorekodi kila mahusiano kwenye daftari lake, kila alipotembea na msichana, jina lake lilikuwa kwenye orodha. Aliweza hata kuwatongoza na kutembea na lecturers wawili wa kike bila uwoga wowote, kuna siku alikuja mzazi wa mwanafunzi mwenzetu ili atoe taarifa za kuuguabkwa mwanae muda mrefu bahati akakutana na mwamba kwenye corridor za chuo mwamba alimwelekeza ofisi zilipo ila baada ya wiki akala na yule mzazi.
Soma: Guinea: Kigogo anaswa na video 400 za ngono na wake wa viongozi mashuhuri, mwanasheria Mkuu aingilia kati
Kuanzia wakati huo, nilianza kumhofia rafiki yangu. Nilihakikisha hajui kuhusu mahusiano yangu yoyote, maana nilihisi hana mipaka. Nilipomuuliza kama alikuwa na "dawa" ya kumwezesha hali hii, alisema hapana, kwamba hilo lilikuwa "la kawaida" kwake.
Mimi kwa upande wangu, katika miaka yote mitatu ya chuo nilikuwa na mahusiano na wasichana 13 tu, na nilihisi kama hiyo tayari ilikuwa zaidi. Baada ya kumaliza chuo, niliamua kuachana na tabia hizi na kuoa.
Rafiki yangu yule alikuwa na akili nyingi, na alikuwa na uwezo mzuri kitaaluma na kijamii pia alikuwa smart sana kimavazi na muonekano wake vilikuwa safi, na alikuwa na mvuto mkubwa kwa watu wengi. Lakini mimi nilijua upande wake wa pili, ambao hata wanaompenda hawakuwa na ufahamu nao.
Kwa sasa jamaa yangu ana cheo kikubwa kazini, na kila tunapoongea namkumbusha kuwa kitu pekee kinachoweza kumuangusha ni tamaa za wanawake. Japo ananiambia amebadilika, bado nina wasiwasi. Kuna watu ambao tamaa zao zimepitiliza katika masuala ya ngono, kama huyu Engonga na rafiki yangu, ambao wanahitaji msaada wa wanasaikolojia ili waweze kudhibiti tabia zao. Maana, ukiwa na tamaa hizi, unaweza kuwa na msichana mmoja leo na dakika tano baadae ukamhitaji mwingine – bila hisia yoyote.