John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 68
- 117
Watu wengine wanakufa kwa kuona aibu ya kwenda kanisani kuombewa uponyaji wa ugonjwa
Uponyaji ni nini
Uponyaji ni tendo la kiimani la kupokea uzima katika roho au mwili kwa njia ya kuombewa, kuwekewa mikono au kulisikia neno sahihi la Yesu Kristo.
Tendo hili la kiimani humletea muumini uzima wa kiroho na afya ya kimwili pale ilipopunguka.
Wengi walipoponywa udhaifu wa miili yao, waliponywa pia na roho zao.
Kumbuka kuwa furushi la uponyaji lilikwishaachiliwa pale msalabani. Maana, Yeye mwenyewe Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, ili tulipokuwa wafu kwa dhambi zetu, tuwe hai kwa mambo ya haki. Kwa kupigwa kwake, sisi tumeponywa (1Petro 2:24).
Uponyaji haufanywi na mtu yoyote yule isipokuwa Mungu. Hata madaktari bingwa, wao hawaponyi bali hutoa tiba tu.
Wanaweza kutoa tiba lakini mgonjwa asipone. Mwenye kuponya ni Mungu. Aidha, watumishi wa Mungu pekee ndiye hufanyika kama daraja au chombo cha kuleta uponyaji ulioachiliwa na Bwana, kwa mhusika mwenye kuhitaji (Mathayo 10:8).
Mfano wa uponyaji wa Naamani Mkuu wa Majeshi ya Mfalme wa Shamu
(2Wafalme 5:1-16)
1 Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
2 Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.
3 Akamwambia bibi yake (mke wa Naamani), laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.
4 Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
5 Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi.
6 Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake.
7 Ikawa, mfalme wa Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu, niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni, basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami.
8 Ikawa, Elisha, yule (nabii) mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.
9 Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha.
10 Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, enenda ukaoge katika mto Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.
11 Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, tazama, nalidhania, bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.
12 Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski (Damascus-Syria) si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.
13 Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, jioshe, uwe safi?
14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika maji mto Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.
15 Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
16 Lakini nabii Elisha akasema, kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Naamani akamshurutisha nabii apokee; lakini akakataa.
Uchambuzi kuhusu uponyaji wa Naamani
Hebu tuchambue mfano huo kuhusu Naamani, Mkuu wa Majeshi ya Mfalme wa Shamu. Huyu Jemedari alikuwa ni mtu mwenye cheo kikubwa, mkubwa serikalini, lakini alikuwa na ukoma (2Wafalme 5:1).
Pia, alikuwa ni muabudu sanamu, yaani miungu wengine.
Fedha zake hazikuweza kumsaidia kuondokana na ukoma. Bali Naamani alimuhitaji Mungu amponye. Laiti kama Naamani asingelikubali kuamini na kutii sauti ya Mungu kupitia nabii Elisha, ni dhahiri kuwa angekufa na ukoma wake, ingawa alikuwa tajiri mwenye fedha nyingi.
Watu wengi wanaumwa kama Naamani.
Kuna watu wanaumwa magonjwa sugu, lakini hawataki kuliamini jina la Bwana Yesu. Wengine wanaona aibu kwenda kuombewa kanisani. Kisha, wanajikuta wanakufa na ugonjwa wao usiotibika hospitalini.
Naamani naye alianza kukataa neno la Mungu kwa sababu ya mitazamo yake (2Wafalme 5:11). Naamani alitaka Mungu afanye vile alivyotaka yeye, na si atakavyo Mungu, kupitia nabii Elisha. Haya ni makosa makubwa, kumpangia Mungu kwa kukataa kile anachokuambia mtumishi wa Bwana.
Hata baadhi ya viongozi wengine na matajiri wengine kama Naamani, sehemu mbalimbali, pia wana shida nzito zinazomuhitaji Mungu aingilie kati. Baadhi yao wanakufa na fedha zao pamoja na shida zao za magonjwa sugu. Maana, fedha au mali haziwezi kumpa mtu wokovu. Yaani haziwezi kuiokoa roho, kama ilivyoandikwa:
“Hapana mfalme aokokaye kwa wingi wa uwezo, wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu. Farasi hafai kitu kwa wokovu, wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake. Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, wazingojeao fadhili zake. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, na kuwahuisha wakati wa njaa. Nafsi zetu zinamngoja Bwana; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu" (Zab.33:16-20).
Fanya uamuzi sahihi kuhusu afya yako.
Hata kama unapitia changamoto gani ya ugonjwa, bado hujachelewa, unaweza kupona. Haijalishi ukubwa au udogo wa umri. Haijalishi ukubwa au udogo wa cheo.
Maana hakuna jambo gumu linalomshinda Bwana, yote yapo katika uweza wake. Kwa Mungu, imani yako ndiyo itakayokuponya, siyo fedha zako. Baadhi ya watu hufa kwa magonjwa na kuacha fedha nyingi kwenye mabenki, huacha pia majengo ya magorofa marefu yamesimama, na msururu wa magari.
Kama una changamoto ya uponyaji wa ugonjwa sugu, muamini Mungu. Tuache kuona aibu kuwa waumini wa dini yako, au dhehebu lako watakuonaje, au watakusemaje ukienda kuombewa kwenye dini au dhehebu lingine tofauti na lako. Ugonjwa ni wako. Ugonjwa wako hauna ubia na mtu mwingine. Ni wako peke yako na utakuua peke yako.
Tukumbuke kuwa MUNGU HANA DINI WALA DHEHEBU. Pia, MUNGU NI WA WATU WOTE. Hivyo, uponyaji wa Mungu haujalishi dini wala dhehebu la mtu. Mtu ye yote anapata uponyaji. Kuwa jasiri. Jipe moyo. Tafuta kanisa sahihi kwa ajili ya maombi ya uponyaji.
Nenda uombewe, na utapona hakika, kwa jina la Yesu Kristo.