mugah di matheo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 6,297
- 12,399
Watu watano wamehukumiwa kifo kwa kumuua Dkt. Sengodo Mvungi
Ikumbukwe Sengodo Mvungi aliwahi kuwa
Mgombea wa Urais kupitia NCCR Mageuzi, pia mjumbe wa kamati ya katiba mpya maarufu kama tume ya Warioba.
Source TBConeline
===
Aidha, Hukumu hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam, mahakama imemuachia huru mshitakiwa mmoja. Inakumbukwa kuwa Marehemu Dkt Sengondo alivamiwa akiwa nyumbani kwake siku ya Novemba 3, 2013 na kujeruhiwa na silaha za ncha kali jambo lililopelekea umauti wake alipopelekwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.
Pia Soma
= > Tanzia: Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa Watu watano baada ya kutiwa hatia kwa makosa ya kumuua aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk.Sengondo Mvungi.
Hukumu hiyo inakuja ikiwa ni miaka 7 tangu watu hao wafikishwe kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Waliohukumiwa ni Msigwa Matonyaz Mianda Saluwa, Paulo Mdondono, Longishu Losingo na John Mayunga.
Pia Mahakama hiyo imemuachia huru Juma Kang'ungu baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Seif Kulita ambapo upande wa mashitaka uliwakilishwa na Mawakili, Credo Rugaju, Lilian Lwetabura, Veronica Mtafya.
Katika kesi hiyo Upande wa Mashitaka uliwasilisha mashahidi 16 na vielelezo 15.
Akitoa hukumu hiyo Jaji Kulita amesema ameridhika pasina kuacha shaka na ushahidi wa Upande wa Mashitaka, hivyo anawahukumu washitakiwa wote kunyongwa hadi kufa isipokuwa mshitakiwa wa Tano ambaye ni Juma Kang'ungu ambaye ushahidi wa mashitaka haumkumgusa.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na washitakiwa hao kufikishwa ni Novemba 22, 2013.
Katika kesi ya msingi washtakiwa kwa pamoja walidaiwa kuwa Novemba 3 mwaka 2013 huko Mbezi Msakuzi Kiswegere walimuua kwa kukusudia Dk.Sengondo Mvungi.
Chanzo: ITV
Ikumbukwe Sengodo Mvungi aliwahi kuwa
Mgombea wa Urais kupitia NCCR Mageuzi, pia mjumbe wa kamati ya katiba mpya maarufu kama tume ya Warioba.
Source TBConeline
===
Watu watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika tukio la mauaji ya Mwanasheria Dkt. Sengodo Mvungi.Aidha, Hukumu hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam, mahakama imemuachia huru mshitakiwa mmoja. Inakumbukwa kuwa Marehemu Dkt Sengondo alivamiwa akiwa nyumbani kwake siku ya Novemba 3, 2013 na kujeruhiwa na silaha za ncha kali jambo lililopelekea umauti wake alipopelekwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.