Wadau nimeona niilete kwenu!
Katika kusaka maisha, kuna jamaa zangu kadhaa ninao wajuwa walifoji cheti; wale jamaa wote sahivi wametusua vibaya! Wana maisha ya maana!
Mmoja alifoji vyeti akaingia bandarini, wengine wizarani, mwingine yupo ikulu aanakula maisha! Yaaani wooote jamaa wapo vizuri;
Imenibidi Leo niwaze sana hivi kwanini mijitu inayofoji vyeti inafanikiwa haraka namna hii jaman!?
Kuna jingine lilifoji cheti sahivi liko tanroad huko mbeya! Yaaani kila sehem ambapo nimewahi shuhudia jitu limeenda na vyeti vya kufoji hakuna hata sehemu moja palikwama!
Mwenzenu nimekata tamaa sitaki tena kusoma; nataka na Mimi nifoji kama mbwai tutajuana hukohuko potelea mbali. Naombeni ushauri wenu wadau.