Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,088
- 4,887
Wale watuhumiwa wa ufisadi na wizi wa mali za umma wengi wapo mitandaoni wanamshauri Mwanamziki Gozibeth asingechoma moto gari bali angewapa wahitaji au kulirejesha.
Kuna baadhi ya wanafiki wamekwenda kutafuta na kifungo cha maisha kwenye sheria kama adhabu wanayotamani apewe.
Baadhi wamekwenda mbali zaidi nakumtukana bila hata kumpa haki yakumsikiliza kutambua tatizo au maamuzi yake yametokana na nini.
Baadhi ya watu wa dini yake wamekwenda mbali sana na kumwacha Mungu na maelekezo yake kisha kujivika hukumu kwamba amelaaniwa. Nani kasema kuchoma magari ni laana? Kwenye biblia gani hii laana imeandikwa?
Mngetumia hii nguvu kupambana na rushwa na ufisadi wa mali za umma mngemsaidia mnyonge asome shule nzuri, tuwe na barabara, tuwe na madawa hospitalini nk.
Enyi mafisadi kataeni rushwa acheni kuwashambulia watu na maisha yao binafsi. Matajiri wangapi wamechoma nyumba na mali zao?
Wezi na mafisadi tulizeni mbongo zenu na mtafakari