GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,190
- 10,316
Msomaji wa Vitabu anafahamu jinsi Vitabu vilivyo na umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku. Vilikuwa muhimu tokea zamani, lakini katika zama hizi, umuhimu umeongezeka mara nyingi sana.
Pamoja na umuhimu huo, kungali kuna idadi kubwa ya Waafrika, Watanzania wakiwemo, ambao hawaupi vitabu umuhimu unaoastahiki.
Kutokuvipa vitabu kipaumbele huenda kumechochewa na kutokufahamu faida zake.
Hiyo ndiyo sababu iliyonipelekea kuanzisha huu uzi, kwa lengo la kuwatia moyo Watanzania wenzangu, kwamba kusoma vitabu vizuri kamwe hakuwezi kuwa upotevu.
Naamini pia humu jukwaani kuna magwiji wenye taarifa zilizoshiba, zao binafsi na za watu wengine walionufaishwa na usomaji wa Vitabu.
Tafadhali ikiwa unafahamu chochote kuhusiana na hilo, naomba uandike humu kwa manufaa ya wengi.
Hawa ni miongoni mwa watu waliofanikiwa kutokana na tabia zao za usomaji.
1. Warren Buffett
Ni C.E.O wa Berkshire Hathaway. Pamoja na umri wake mkubwa, miaka 92, bado anatumia asilimia themanini ya muda wake kusoma vitabu.
Alianza kusoma vitabu tokea akiwa na miaka 7, na ameendelea na hiyo tabia mpaka uzeeni mwake.
Anahusianisha mafanikio yake na tabia ya usomaji.
Alipoulizwa jinsi ya kufanikiwa, alishauri kusoma kurasa 500 za kitabu kila siku. Maarifa mtu anayojikisanyia hatimaye yatakuwa sehemu ya maisha yake.
2. Dr. Ben Carson
Wakati akiwa madarasa ya chini, aliaminika kuwa ndiye mwanafunzi kilaza kuliko wote darasani kwao. Hata yeye aliamini hivyo pia.
Jitihada za mama yake kumlazimisha kusoma Vitabu kulizaa matunda. Miezi kama sita baada ya kuuanza huo utaratibu, kulimpelekea kufanya ugunduzi mkubwa sana maishani mwake, kwamba yeye naye ana akili.
Ugunduzi huo ulimfanya ainuke kitaaluma, kutoka kuwa mkia hadi kuongoza darasani. Baadaye alikuja kuwa daktari bingwa aliyesaidia wagonjwa wengi ndani na nje ya Marekani.
3. Mohamed Said
Simfahamu sana huyu mzee. Nimeanza kusoma makala zake Jamii Forum hivi karibuni. Makala chache nilizozisoma zimenihakikishia kuwa ni msomaji mzuri wa Vitabu. Nina uhakika kuwa ni kati ya watu walio na mafanikio katika maisha yao.
Bado sijafanikiwa kukisoma kitabu alichokiandika, lakini hakitaweza kunipiga chenga. Nitavitafuta.
4. Bill Gates
Pamoja na kuwa na mambo mengi, bado anajitahidi kusoma vitabu visivyopungua 50 kwa mwaka.
Anakiri kuwa Vitabu ndiyo chanzo kikuu cha maarifa yaliyomwezesha kuwa na mafanikio makubwa kiuchumi.
5. Eric Shigongo.
Naamini wengi wanamfahamu. Yeyote aliyewahi kufuatilia Historia ya maisha yake, atakubaliana nami kuwa mtaji mkuu wa mafanikio yake ni Vitabu.
Sijawahi kukutana naye ana kwa ana, lakini nilifanikiwa kusoma makala kadhaa yanayohusu maisha yake na mafanikio. Nilishakisoma na kitabu chake kinachofundiaha na kuhamasisha mafanikio.
Kwa ufupi, yuko vizuri kichwani.
Shigongo ni mfanyabiashara na mbunge katika Bunge la JAMHURI ya Muungano wa Tanzania. Na kama nilivyosema, mafanikio aliyo nayo, msingi wake mkuu ni usomaji Vitabu.
5. Christopher Mwakasege
Ingawa ni Mchumi kitaaluma, lakini pia ni Mhubiri. Ameshaandika Vitabu vingi, hasa vya mafundisho ya Kikristo ambavyo baadhi vina mwelekeo wa Kiuchumi. Wasomaji wa Vitabu wanafahamu kuwa waandishi wazuri wa Vitabu ni wasomaji wazuri pia. Ukisoma Vitabu vyake utang'amua kuwa ni msomaji mzuri.
6. Julius K. Nyerere
Huyu naye alifanya urafiki na Vitabu. Mzee Said Mohamed alishawahi kuandika makala yaliyoonesha kuwa baba wa Taifa alikuwa ni mtu wa Vitabu.
Naamini hata mbinu alizozichagua kutumia wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika, kulichagizwa na usomaji wake wa Vitabu. Aliufahamu vyema ulimwengu wa wakati wake.
7. Richard Branson
Ni mmoja wa mabilionea wa Uingereza. Aliacha shule akiwa na miaka 15, lakini hakupeana talaka na vitabu. Anakisifia kitabu cha kiuchumi kiitwacho SMALL IS BEAUTIFUL kuwa ndiko alikopata mawazo yaliyofanya mapinduzi katika biashara zake. Ni kawaida yake kutembea na notebook kwa ajili ya kuandika mawazo mapya anayoyapata kwa njia mbalimbali ikiwemo Vitabu.
8. Tony Robbins
Alipokuwa High School, alikuwa ameshasoma zaidi ya Vitabu 500, vingi vikiwa vya Saikolojia.
Kupitia Usomaji, alijikusanyia maarifa aliyokuja kuyageuza kuwa mtaji na hatimaye kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio makubwa sana ulimwenguni.
Kwa mifano hiyo michache, ni wazi kuwa tokea zamani hata sasa, Vitabu vimeendelea kuwa na umuhimu mkubwa sana katika kuchochea maendeleo.
Naomba kuwasilisha.