African businesses
Member
- Feb 13, 2024
- 68
- 175
Mambo sio kama zamani tena katika jamuhuri ya watu wa Giningi, wanaginingi wanajiuliza maswali mengi yasio kua na majibu, mwanzo jamuhuri ya Giningi ilijipatia sifa tele pande zote za dunia hii, jamuhuri ya watu wa Giningi ilikua ni mfano wa kuigwa kutokana na amani na upendo wa watu wa Giningi.
Lakini leo wanaginingi wanajiuliza maswali mengi na bado hawapati majibu, wanaginingi wanajiuliza ni nani anayewateka ndugu na jamaa zao ila wanishia kujibiwa ni watu wasiojulikana, wanaginingi wanajiuliza ni nani aliyewafanya vijana wa Giningi kuwa machawa walaibu wa kubeti na walevi wa pombe chafu lakini hawana majibu, wanaginingi wanajiuliza ni nani aliyewaleta viongozi ambao hawajali masilai na utu wa wanaginingi still bado hakuna majibu
Mwanagingi mmoja kaenda mbali na kusema tangia kuanzishwa kwa jamuhuri ya watu wa Giningi hajawai kushuudia kiongozi mwenye upendo kwa wanyama kama huyu Bibi Kilembwe kiasi kwamba anawahamisha raia wa Giningi kutoka kwenye eneo lao ili wanyama waishi kwa raha mustarehe.
Ni kweli wanaginingi wana maswali mengi yasio kua na majibu, wanaginingi wanawalalamikia viongozi wao wa dini hawana maadili kama wale wa zamani, wanawalalamikia wasanii hawana maadili kama wale wa zamani, wanawalalamikia viongozi wao hawana maadili kama wale wa zamani.
Lakini jambo wasilolijua wanaginingi hawa wachungaji, wasanii, viongozi wanaowalalamikia kukosa maadili ni sehemu ya wanajamii wa Giningi na kama ni hivyo basi tatizo lipo kwa wanaginigi wote, yahani hawa wasanii, wachungaji na viongozi ni reflection ya kilichopo ndani ya wanajamii wa Giningi, ukipanda mahindi chini ya aridhi, aridhi itakutolea mmea wa mhindi na si vinginevyo.
Kama wana Giningi wanataka kumaliza hizi changamoto lazima wajikite kwenye mzizi wa tatizo na sio kuangaika na matokeo ya tatizo, kuna mahali wanagingi walikosea, haswa katika mifumo inayowaandaa raia waginingi kama vile elimu, suala zima la maadili matokeo yake jamii inatoa watu ambao ndio products ya jamii hii ya watu wa Giningi.
Mwisho kabisa nipende kuwaaga na salamu maalum ya wa watu wa Giningi, jamuhuri ya watu wa Giningi nyie mnamalizia kazi iendelee.