Watu wa HipHop wote tukutane hapa-Nas Escobar, Common,Jadakiss & Styles P

Golden Age

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
203
45
WHY??? - JADAKISS,COMMON,STYLES P & NAS
Ukisikiliza album ya " Kiss of the death"ya Jadakiss utakutana na track inaitwa "why" moja ya ngoma iliyozua utata na mvutano mkubwa kati ya Jadakiss na uongozi was America. Ni track ambayo kwa 40% ilikua ikielezea position ya mtu mweusi America.

Ngoma ilikua Kali sana mdundo ulipigwa na havoc,so ikatoka remix yake ambapo akashirikishwa common,Nas na Styles P. So ebu tuchec washkaji waliandika nini humo ndani.

Styles P alisikika akichana"why is garbage music selling a lot?/Why is the music industry state of mind real far from Hiphop. Pia anaongezea kwa kusema " the revolution will not be televised if around here".Hapa styles P anadai muziki wa kupotosha jamii unapewa support kubwa ukilinganisha na Hiphop,so styles P anadai system ya america kwa makusudi kabisa inakwamisha Hiphop na harakati zote zinazohusiana na kumkomboa mtu mweusi.Styles P sio mtu wa kwanza kuongea hii issue ma emcee wengi tu wameshaongea hii issue Mara nyingi tuu.

Pia anasema " why vote Republican if you black" Hapa anaelezea uhalisia wa chama cha Republican,ambacho kimekua kikihusishwa na ubaguzi wa rangi,na sehemu kubwa ya jamii ya watu weusi hawakisapoti na kukipigia kura chama cha Republican akiwemo na styles P mwenyewe.Pia anasema " why build more jails less schools cause we under attack".Hapa Styles P anaeleza jinsi marekani ilivyowekeza sana katika vyombo vya usalama,mahakama na magereza ili kumkandamiza mtu mweusi,pamoja na kuyakandamiza mataifa mengine.Polisi,mahakama na magereza ndo nyenzo kuu za kumkandamiza mtu mweusi america.


Pia common anasikika akisema " why you kill on every song?/why you frown at the screen/.Hapa Common anadiss marapa wa gangsta rap,ukifuatilia gangsta rap watu huwa wanaiita ni " government rap" kwamba ulikua ni mpango wa marekani kumkandamiza mtu mweusi. Hii issue ya gangsta rap tutakuja kuidiscuss kwa undani zaidi siku nyingne.

Pia Jadakiss alisikika akichana" why they gonna give you life for murder/ Turn around only give you eight month for a burner/. Jadakiss anadai adhabu wanayopewa watu ambao wamethibitika kumiliki silaha kinyume na sheria ni ndogo mno ndo maana tatizo la uhalifu wa kutumia silaha" gun violence " haliishi Marekani.

Pia akichana akisema " too many thrones why we argue who is the king".Kwamba Hiphop haijawahi kua na mbabe kwa sababu unaweza ukasema Krs one ni mkali,lakini pia Rakim,K- rino,Guru,Immortal technique na wengine wengi ni wakali sana tuuu.


Pia Jadakiss anachana"why they kill 2 PAC and Chris " Chris anamaanisha Christopher Walles,Jadakiss anaamini CIA pamoja na serikali ya marekani ndo waliomuua 2 PAC na Biggie Notorious.

Pia alisikika akichana"Why did Bush knock down the towers "Jadakiss anaamini Bush anahusika katika kulipua jengo la world trade center ile 9/11.Huu mstari ulizua utata mkubwa sana mpaka baadhi ya wanachama wa Republican wakatangaza Kwamba Jadakiss ashitakiwe kwa mstari wake aliomdiss Bush,na hii ikasababisha hii ngoma ifungiwe kwa sabab ni ya kichochezi,lakini kuna zile redio za maniga Hiphop ambazo hua zina play Hiphop Masaa 24,ziliendelea kuiplay hii ngoma kama kawaida.


Pia common anachana " why Bush acting like trying to get Osama/why don't we impeach him and elect Obama./ Hapa Common alitabiri Obama atakuja kua Rais na utabiri wake ukatimia,kipindi hicho Obama bado Senator Illinois.

Common pia anachana " why I gotta have religion if I believe in God" .Common haamini sana katika dini ila yeye anachojali ni mahusiano yake ya moja kwa moja na Mungu.Dini haikuokoi ila kinachokuokoa ni mahusiano yako mazuri na mwenyezi Mungu.Dini ndo imesababisha watu watengane na kuuana baina ya watu wa dini tofauti.Watu wote wameumbwa na Mungu...na kinachoangaliwa ni watu sio dini,ni Kama sahani ya pilau,kinachoangaliwa ni pilau na sio sahani iliyobeba pilau.

Nas pia alileta utata kwenye verse yake akichana "Why is Jesus Christ never played by black actors" Hapa ndo unakuja ule utata je Yesu alikua mtu mweusi?????? Hapa hua namkumbuka Jacob Makalla (Jesus come black) Kuna watu wanaamini Yesu alikua mtu mweusi.Mambo ya dini hayo kila mtu na imani yake.....itaendelea

Muendelezo utakuepo katika kitabu cha HipHop na Maisha ambacho kitatoka hivi karibuni na unaweza ukaweka oda kupitia namba 0713560346 / 0743959819

Asanteni sana.....

Naomba kuwasilisha...
 
Why remix
 

Attachments

  • Jadakiss+-+Why+%28Remix%29+Ft.+Styles+P%2C+Common%2C+Nas+%26+Anthony+Hamilton+%28+240+X+320+%29.mp4
    9.5 MB · Views: 34
The System was designed to undermine the black community all around the world....emphasis on ALL AROUND THE WORLD...ndo maana most rappers wanajaribu kutufungua macho kwa sababu bado tumetekwa na bado sisi ni watumwa so dhumuni kubwa la Hip Hop ni kujaribu kumkomboa mtu mweusi katika huu ulimwengu uliojaa vitu vya Mzungu...hata Kanye alisema"...is Hip Hop just a Euphemism for a new religion, the soul music for the slaves that the youth is missing..."...so kila ukitikisa kichwa jaribu kusikiliza kwa umakini ujumbe wa ukombozi uliokatika mziki huu tuupendao.
 
Kweli kabisa mkali Havoc
 
Mkuu uchambuz wako umekaa poa sana lakini ni vizur kushare na cc hapa hapa kuliko kitabu ambacho ni waz hakita wafikia watu wengi!
 
Mkuu kuna shida kidogo kwenye ku upload labda unitumie message hapa 0713560346...nikutumie mizigo yote miwili
Wewe unayeandika kitabu cha hiphop ni nani hasa mpaka tukinunuwe....au huyo mtunzi ni nani hasa tukisubiri kitabu kwa hamu zote?
Au kimeandikwa na styles p au nassir jones au common?
 
Hapo kwenye gangster rap sikuungi mkono.
Ila nacho weza kusema Kiss is underrated.
System inatumia nguvu nyingi kuharibu utamaduni wa Hip Hop.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…