Watu saba wamefariki dunia na wengine 75 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea wilayani Same

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
14,691
24,404
Watu saba wamefariki dunia na wengine 75 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea wilayani Same. Ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Njoro na kuhusisha basi la Kampuni ya Osaka lililokuwa likielekea Dar es Salaam, ambapo ilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 52 walijeruhiwa.

Ajali ya pili ilihusisha basi aina ya Costa la Kampuni ya Mkokota majira ya saa2 asubuhiya leo, ambalo lilipinduka katika kona za milima ya Ilamba, na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi 23. Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni wanakwaya waliokuwa wakisafiri kutoka Chome kuelekea Ndolwa.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same, Dkt. Alex Alexander, amesema kuwa majeruhi wa ajali ya kwanza walipokelewa hospitalini majira ya saa nane usiku, huku majeruhi wengine 23 pamoja na miili ya marehemu sita ikifikishwa hospitalini mchana wa leo.

IMG-20250330-WA0087-1536x1024.jpg



View: https://youtu.be/D_2maGWZn4Y?si=_QUdY4lhQHgOjcfN
 
Sema wanakwaya wana mikosi sana kupandq gari moja ,hivi karibuni walikufa hapo wanakwaya ..Leo katika wale 7 ,sita ni wanakwaya.
 
Akimaliza kuchinja chap atafika eneo la tukio hivyo msiwe na mashaka yupo pamoja na wana Chame
 
Sema wanakwaya wana mikosi sana kupandq gari moja ,hivi karibuni walikufa hapo wanakwaya ..Leo katika wale 7 ,sita ni wanakwaya.
Mwaka ule wanakwaya walikufa Njombe ilikuwa kipindi kama hikihiki kuelekea Pasaka
 



30 March 2025

WANAKWAYA 6 WAFARIKI DUNIA, 75 WAJERUHIWA AJALI MBILI TOFAUTI SAME

Watu Saba wakiwemo wanakwaya Sita wamefariki dunia papo hapo huku wengine 23 wakijeruhiwa baada ya gari walikokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kupinduka katika milima ya Pare, Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Same, DC Kasilda Mgeni amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, ambapo amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi majira ya saa nne, Machi 30, 2025 eneo la barabara ya Bangalala wakati wanakwaya hao wakitokea Chome kuelekea Vudee wilayani humo.

"Leo majira ya saa nne katika barabara ya Bangalala, Wilaya ya Same, kumetokea ajali ya gari aina ya coaster lililokuwa limebeba wanakwaya ambao walikuwa wanatokea Chome kuelekea Vudee, ambapo wanakwaya 6 wamefariki duniani na kusababisha majeruhi 23,"amasema DC Mgeni

Aidha amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari walikokuwa wakisafiria kufeli break na kupoteza mwelekeo na kupelekea kupinduka katika milima hiyo.

"Hawa wanakwaya walikuwa wamepanda gari aina ya coaster sasa walipofika barabara ya Bangalala gari lilifeli break na kuanza kurudi nyuma nyuma na ndipo liliposerereka na kupinduka na kusababisha vifo vya wanakwaya Sita na majeruhi 23,"amesema DC Mgeni.

DC Mgeni amesema miili ya wanakwaya hao, imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Same.

Akitoa salamu za pole kwa familia hizo, DC Mgeni amesema wanaendelea kuziombea familia ambazo zimepoteza wapendwa wao na kuwaombea subira katika kipindi hiki cha majonzi."Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu amina."

Katika tukio jingine, mtu mmoja amefariki dunia huku wengine 52 wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Moshi kuelekea Dar es salaam kupata ajali katika eneo la Njoro, wilaya Same.

"Kuna ajali ya pili ambayo imetokea eneo la Njoro majira ya saa 7 usiku, ajali hii inahusisha basi lililokuwa likitokea Moshi kuelekea jijini Dar es salaam ambapo watu 52 wamejeruhiwa na mmoja amepoteza maisha,"amesema DC Mgeni

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Mkoani hapa.Mwisho
 
Back
Top Bottom