Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia katika ajali ya gari baada ya basi la kampuni ya Nyehunge kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Asante Rabi.
Ajali hiyo imetokea leo Oct 22, 2024 majira ya alfajiri katika eneo la Ukiliguru, wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
===
Watu wanane wamefariki dunia na wengine 39 kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha mabasi mawili ya Kampuni ya Nyehunge lililokuwa linatokea Morogoro kwenda Mwanza na Asante Rabi lililokuwa linatokea Mwanza kwenda Arusha, baada ya kugongana katika eneo la Ukirigulu, Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza mapema alfajiri ya leo October 22, 2024.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa za ajali hiyo amesema idadi ya Watu waliofariki kwenye ajali hiyo awali ilikuwa Watu watano lakini vifo vimeongezeka na kufikia Watu wanane.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la Asante Rabi lilipokuwa likijaribu kulipita gari jingine kabla ya kukutana na basi la Nyehunge na kusababisha ajali hiyo.
Millard Ayo