Watu maarufu (Wanasayansi, Wasanii, Wafanyabiashara, Wanamichezo) wazee wa kataa ndoa duniani

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,683
14,051
Twende nami taratibu.

Baada ya kuwatazama Marais wa wakataa ndoa duniani sasa ni zamu ya watu maarufu walio nje ya ulingo wa siasašŸ˜Ž

1. Oprah Winfrey
Ukurasa unafunguliwa na huyu ajuza vijana wa kisasa wanasema shangazi.

Huyu legend wa kike ni mwanaharakati haswa wa wazee wa kataa ndoa.

Huyu legend hajawahi onesha interest yoyote ya kuzama ndoani pamoja na umri wake kukimbia haswa miaka 70 sasa.

2. Isaac Newton
Haya namba mbili tumzungumzie legend wa fizikia duniani.

Sio tu u legend wa fizikia pia huyu mwamba alikuwa mwanachama.mtiifu wa kataa ndoa katika kipindi cha uhai wake hakuna rekodi yoyote ya yeye kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi na mwanamke.

Kwa mujibu wa historia mwamba namna alivyo zaliwa ndivyo alivyo kuwa kufa alitumia zaidi ubongo kuliko kiungo kingine katika mwili.

Kweli huyu alikuwa legend haswa wa wazee wa kataa ndoa.

3. Leonardo Da Vinci
Huyu alikuwa msanii maarufu wa kiitaliano nafikiri hata sehemu kubwa duniani anafahamika kwa picha yake ya monalisa

Huyu mtaalamu alikuwa mwanachama mwaminifu wa wakataa ndoa kote duniani.

Mpaka anakufa hakuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

4. Galileo Galilei
Huyu bwana alikuwa mwanasayansi wa kale.

Huyu mwanasayansi mkonge aliyeleta mapinduzi kwa wazungu huko ulaya hakuwahi kuoa alikuwa ana miliki kadi ya wanachama wa kataa ndoa na alikuwa balozi wa wakataa ndoa toka kale.

5. Nikola Tesla
Huyu alikuwa mwanasayansi au unaweza muita injiania wa kiserbia.

Huyu legend naye alikuwa na tabia kama za Isaac Newton huyu bwana yeye katika kipindi chote cha maisha yake hakuwahi kabisa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke yoyote yule.

Huyu alikuwa legend wa wakataa ndoa duniani kote.

Wengine wa sasa ni kama
6. Leonardo DiCaprio
7. Christian Ronaldo
8. Mayweather
9. Elon musk
10. Bill Gates

list ni ndefu ongeza na yako list pia inaweza badilika kutokana na majina tajwa wakibadili maamuzi.
 
Kubali NDOA, Ndoa ni agano kati ya mwanamke na mwanaume, Ndoa ni ishara ya kumtambua mwenyeezi Mungu, Ndoa ni taasisi kama ilivyo serikali yoyote duniani.

kubali NDOA, Ndoa ndiyo shule, chuo kikuu bora duniani ambacho muhitimu wake anapewa cheti siku ya kwanza kabla hajaingia darasani.

kubali NDOA, usikatae Ndoa, uzao wote duniani umetokana na mahusiano ya Ndoa, watoto wanaozaliwa nje ya Ndoa ni watoto na wanatambulika ila hawana nafasi ya wazazi kuwa wenye Ndoa.

Usikatae Ndoa, huwezi kuelewa kwa nini sheitwan anapambana kuharibu taasisi hii kubwa kwa vibweka lukuki..?.

Kubali NDOA jengo kesho inayoeleweka na kuheshimika kwa kizazi kijacho.

NDOA haina furaha, upendo sababu tumemuachia ibilisi aisimamie.
 
Back
Top Bottom