Watu hatari zaidi katika kuwa nao ni hawa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
4,102
4,228
Ni vizuri kuwa na marafiki wa aina mbalimbali kwa mtu lakini ni vizuri zaidi kuelewa aina ya marafiki ulionao. Kuwa na idadi kubwa ya marafiki siyo sababu ya mtu au Taifa kujiona linapendwa au lina msaada fulani kutokana na idadi ya marafiki. Urafiki ni muhimu ila kuelewa aina ya urafiki na namna ya kuendeleza urafiki ni muhimu zaidi.

Ni vizuri kila mtu mtu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa akiweza kujifunza kuweka mipaka ya urafiki katika maisha yake. Kuweka mipaka hakumaanishi kuwachukia wengine ila kuchuja na kuhakikisha misingi haivurugwi.

Marafiki wafuatao; Wambea (Gossiper s), Waalimu wa uongo(False teachers), Wenye dharau/dhihaka (scoffers), Wanaokuweke mitego/wajaribu(Tempters) na Wabinafsi ni watu ambao unapaswa kuishi kwa hadhari kubwa sana unapokuwa nao. Simaanishi uwatenge ila ujihadhari sana kuwa nao kwa sababu watu wa aina hii ni sawa na sumu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.

 Wambea - Hawa hueneza habari zozote zile zisizo na uhakika kwa kujua au kutojua. Kujifungamanisha sana na watu wa aina hii kinaweza kukuingiza kwenye matatizo taratibu na mwisho ukajikuta ndani ya dhahama kubwa.

Walimu wa uongo- Hawa hujihusisha na kueneza maarifa pototofu, wakati mwingine siyo rahisi sana kuwabaini kwa sababu wanajificha kwenye kufundisha na kurithisha maarifa. Wanaweza kuonekana kama ni watu wa muhimu katika jamii kutokana na ushiriki wao katika kuielimisha jamii masuala mbalimbali( kiuchumi, kisiasa, kijamimi n.k) ila katika mafundisho yao huipotosha jamii Kwa ujanja sana. Waalimu wa aina hii wapo katika nyanja zote za kijamii na Kwa kujua au kutojua huwa sehemu ya kuipotosha jamii.

 Wajaribu- Hawa ni aina ya watu ambao huwashawishivkwengine kufanya upotofu na kuivunja miiko au misingi yao. Hawa hutumia nguvu ya ushawishi kutafuta wafuasi wao katika upotofu.

Wenye dharau -Hawa kazi yao ni kukupuuza tu, hakuna utakachokifanya wakakupongeza Kwa sababu lengo lao ni kuhakikisha haujithamini.

Wabinafsi -Aina hii ya watu ni wake wenye kujiangalia wao tu, maslahi yao kwanza.

Ukibaini unaishi na watu wa aina hiyo popote pale jizoeshe kuweka mipaka mapema hata kama ni ndugu wa karibu kiasi gani. Kuweka mipaka yako siyo kuwatenga ila kuishi nao Kwa hadhari.
 
Back
Top Bottom