Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,334
- 4,726
Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Khudheifa Changa, ambaye alikuwa ni Muuguzi wa Hospitali ya KCMC Moshi mkoani humo.
Inadaiwa Khudheifa Changa aliuawa usiku wa kuamkia Julai 2, mwaka huu wakati akipita katika uchochoro wa Mtaa wa Marindi mjini Moshi, katika purukushani alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mbavu ya kushoto usawa wa moyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Simon Maigwa, amesema kuwa watuhumiwa hao ambao watatu ni wanaume na wanawake wawili walikuwa na nia ya kumpora mali alizonazo, na kwamba watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
Pia soma: Muuguzi KCMC auawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali uchochoroni