Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
123,593
234,221
Watu wanne wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 19, 2024 wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashktaka mawili.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Kanda Dodoma na kusomewa mashtaka ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa jina lake mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania mkoani Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu.

Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi

Kwa mujibu wa taarifa ya Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia leo Agosti 19 hadi Agosti 23 siku ya Ijumaa.

Pia soma:

1. Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu

2. Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa

Screenshot_2024-08-19-17-36-45-1.png
 
Back
Top Bottom