A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na vitendo vya ufisadi unaofanywa na baadhi ya watumishi wa manispaa ya Ubungo kitengo cha wakusanya ushuru pale stendi ya mabasi Magufuli.
Wakusanya ushuru Hawa kwa kushirikiana na wasimamizi wao wa stendi pamoja na baadhi ya watumishi makao makuu Ubungo manispaa kitengo cha fedha na uhasibu wamekuwa wakichukua pesa bila kutoa risiti kwa wananchi au wateja wao na mwisho wa siku kugawana mapato hayo.
Nashauri ofisi ya Raisi TAMISEMI ilifanyie jambo hili uchunguzi wa kina na hatua zichukuliwe kwa wahusika.
Pia soma ~ Miundombinu ya mabomba kwenye Vyoo vya 'Magufuli Bus Terminal' imeharibika, maji yanatoka hovyo na hakuna anayejali