Habari wana harakati,jamani sijui nani kaliona hili tatizo la watoto wa mtaani ambao sasa wemekuwa wakubwa vijana wa mtaani,ukisimama kwenye mataa ya barabarani wanakuja kufuta kioo ,hata kama gari ni safi unashangaa tu umeshamwagiwa maji ya mapovu pwaaaa
,jamani uwa unatamani sijui ufanye nini,mimi uwa nawaambia,wadogo/wanangu haina haja unisafishie kioo ndio nikupe pesa maana nimekuja na gari langu safi wewe nigongee kama nina pesa nitakupa kama sina siku ingine,okey tatizo zaidi ni hawa watoto kukulia mtaani wakiwa vijana,je hii tunazalisha nini hapo baadae,na nani ni muhusika wa hawa vijana jamani,nani anaweza kuwasaidia,au wizara gani husika jamani,najua wananchi yatupasa na sisi tushiriki kwa kiasi kikubwa lakini sasa wizara au taasisi flani husika ijitokeze ili wananchi tuje tuweke nguvu zetu hapo kuwasapoti,jamani inakasirisha na inaumiza,hawa vijana wako kwa wingi pale mataa ya maeneo ya Serena hotel,na barabara ya Nyerere road karibia na Tazara.
Wahusika tusaidie hawa vijana ni wengi mnoooooooo,na wengine ni watoto wanakulia humo humo,mbali ya hawa omba omba wanaokaa pale mnazi mmoja na watoto wao au pale junction ya kwenda oysterbay na kinondoni.Msaada wa haraka hawa watoto tusije wapoteza wengi katika ujangili au mambo mabaya zaidi.