Watoa huduma kwa Wateja wa TTCL hawajanihudumia vizuri

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,005
42,399
Habari wana JF, ninaomba msaada wenu, kama kuna mtu mwenye namba za simu za top management staff wa shirika tajwa anisaidie, nimekuwa mteja wa TTCL kwa miaka kadhaa lakini ninashangazwa na jambo moja na hasa kuhusu customer care zao, nilipeleka taarifa kuwa sipati huduma ya mtandao kwa muda mrefu pamoja na kuwa nimelipia bili zangu zote.

Pamoja na kufika ofisini kwao zaidi ya mara nne, wamekuwa ni watu wa ahadi lakini hawatatui shida yangu, mbaya zaidi wapo wateja wenzangu wenye shida kama yangu waliambiwa wandike barua ya kulalamika ili washughulkie shida yao, yapata mwezi na wiki kadhaa sasa huduma hazipo.

Je Customer care wapo kwa ajili ya nani? viongozi wa shirika husika mpo kwa ajili ya nani? nauliza maswali haya kwa sababu ukifika idara ya huduma ya wateja hawatatui shida za wateja, ukiomba kuonana na wakubwa wao, kamwe hawakuruhusu, ukipiga simu ili wakuunganishe na wakubwa wao, wanakuuliza unashida gani, ukiwaambia wanasema hiyo shida haiwahusu management.

Nashauri kama MD wao unapata habari hii, utambue kuwa shirika lako linamalizwa na watendaji wako, wewe pamoja na management staff wenzako mpo mbali na wateja, wekeni anuani ya wazi ili kuwawezesha wateja wenu kuwasiliana nanyi moja kwa moja kwa sababu anuani yenu ya info@ttcl.co.tz na namba zenu za simu
  • Telephone: +255 22 214 2000
  • FAX: +255 22 214 2045
  • E-mail: info@ttcl.co.tz
  • Toll Free: 100.
  • Corporate Customers toll free: 140.
  • NICTBB toll free: 144 / 0800 11 55 55.
  • Directory enquiries toll free: 135
mlizoweka pamoja na barua za malalamiko tunazofikisha ofisini kwenu tena kwa mkono havina msaada wowote, tell us, who are you there for?
 
Pole sana mkuu.....
Shida ni shirika la umma, ili liwe na ufanisi lazima walifanyie overwhelming kuanzia sheria ilioliunda au wajifunze toka China au Vietnam au crdb( marketing and customer care)
 
Pole sana mkuu.....
Shida ni shirika la umma, ili liwe na ufanisi lazima walifanyie overwhelming kuanzia sheria ilioliunda au wajifunze toka China au Vietnam au crdb( marketing and customer care)


Nashukuru Mkuu, ni kweli kwa sasa halina tofauti na mtumbwi uliotelekezwa baharini
 
Kwa shirika kama hilo mtu ukihudumiwa vizuri ndio inapaswa kuwa ajabu na habari.... hiyo yako ni kawaida
 


kazi ipo kwakweli,
 
Hii taarifa ingemfikia Mh Prof. Makame Mbarawa nafikiri ingekuwa vyema zaidi. Kuna siku alikuwa TTCL HQ aliwaasa kuhusu Huduma zao mbovu na suala la kujipanua kiushindani wa kibiashara.
 
Ni kweli TTCL bado mna shida. Nimefuatilia huduma za NMB mobile hakuna mwenye jibu. Tunapoteza fursa. Changamkeni TTCL
 
Hawajali kabisa, hebu tazama hii ndiyo sakafu katika moja ya regional ofices, sijui walitumia mafundi kutoka wapi!!!?
 
Pole sana kwa changamoto.
Tafadhali tufahamishe ulihudumiwa ofisi ya TTCL tawi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…