Wateule wa Hayati Magufuli hawamfai kamwe Rais Samia Suluhu, hawakuwa na huruma wala utu

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,322
2,105
Samia alichoshindwa kuelewa ni kuwa pamoja na kuwa alikuwa ni Makamu wa Rais hakuumbwa kuwaza au kufikiri au kutenda au kunena au kufanya kitu chochote kama alivyokuwa Mtangulizi wake.

Kwanza namna alivyowekwa pale na majukumu ya Makamu yalivyo KiKatiba alikuwa ni mtu passive tu - yaani kuangalia tu kilichokuwa kikitendwa na JPM bila yeye kuingilia au kufanya chochote.

Kwanza haikutegemewa kamwe kama Mwenyezi Mungu angeleta uamuzi ule na hivyo hakuna aliyewahi kufikiri kuwa Samia atakuja kuwa Rais wa nchi hii. Aliyekuwa anajua hilo ni Mwenyezi Mungu pekee

Samia, Rais, wangu - nilikushangaa sana ulivyoanza kuwapa nafasi muhimu watu ambao wanajulikana kabisa kuwa nia yao ni kushika Urais. Hakuna asiyejua nchi hii mtu kama Mwigulu alipania sana kuwa contestant wa URais kwa mwaka 2025 na sasa haamini kama kufikia 2030 umaarufu wake utakuwa ni uleule. Hivi SSH ni kweli kabisa unaamini Dr. Mwigulu alifaa kushika hiyo nafasi? Kweli kabisa uliamini hivyo.

Waziri wa Fedha hata awamu zilizopita alikuwa anachukuliwa mtu ambaye hakuonekana kamwe kuwa na dalili za kutaka uongozi wa juu wa nchi. Hapa Dr. Mwigulu hakuwa nafaa kabisa kwa sababu Waziri wa Fedha hapaswi kuwa mtu wa kubadilika badilika. Mf. mdogo ni Dr. Mpangao, huyu bwana pamoja na kuwa katika Serikali ya Jiwe lakini alikuwa ni mtu wa kusimamia zile principles za kifedha na hakuweka siasa nyingi sana kwenye hilo na ndiyo maana alidumu na isitoshe hamna hata mtu alimfikiria kuwa atakuja kuwa Makamu wa Rais. Kwa Mpango mama ulipiga bingo sana hata watu wengi kama walimtaka Majaliwa.

Sasa kwa huyu Mwigulu kigeugeu kwa hakika hutakaa usifiwe au upongezwe kama uliweka Waziri wa Fedha makini. Huyu mtu ni kinyonga huyu. Anabadilika na hana msimamo wake - anapenda kwenda na upepo na anatategemea wataalamu ambao wamebeba agenda za kisiasa.

Yeye mwenyewe hana msimamo wake unaoeleweka kwenye principles za uchumi. Kama anazo hebu tuambieni ni zipi? Dr Mpango tangu akiwa World Bank na hata Tume ya Mipango amekuwa akionekana kabisa ni mtu wa kutamani kukuza uchumi wa watu duni.

Hata kataika regime ya JPM pamoja na kujenga mamiundombnu lakini Mpango mara zote alikuwa akiongelea theories za kuinua wanyonge! Dr. Mwigulu huyu mwenye Phd ya juzi juzi tu na isiyoeleweka vizuri mnataka kutuambia principles zake hasa ni zipi?

Leo hii hata ukiamua kumweka Dr. Kimei kuwa Waziri wa Fedha waTanzania tutajua kabisa huyo Waziri atatupeleka kwenye kujenga uchumi kwa kupitia principles gani? Ukimchukua hata Prof. Mkenda yule Waziri wa Kilimo utaona kabisa anaweza kujipambanua kwa principles gani za uchumi

Hivi mama Samia ni vigezo vipi vilikufanya umchukue Dr. Mwigulu ambaye hakukaa sana kwenye Unaibu wa Wizara ya Fedha kuwa Waziri wa Fedha?

Huyu bwana alifanya kazi Benki Kuu kama Afisa tu wa kawaida na alikuwa Mwanaharakati kweli kweli na hakuwa hata mtendaji mzuri leo hii eti mnamfanya Waziri wa Fedha.

Huyu mtu hafai na asikupime Mhe. Rais wetu mwambie tu kisirisiri ajiuzulu ili huko baadaye umpe nafasi ingine! Akigoma kufanya hivyo TUMBUA una wengi wanafaa nafasi yake.

Hapo nimemsema Dr. Mwigulu tu lakini una mawaziri wengi tu ambao hawakufaa kwenda na wewe! Mungu kakutofautisha na wengine so unapaswa kufikiri kwa kadri Mwenyezi Mungu anavyokuongoza.

Wewe umeletwa kwetu na Mungu Mwenyewe wala sio na JPM, CCM au wapinzani. Ni Mwenyezi Munhu mwenyewe kakuleta sikiliza Mwenyezi Mungu anavyokuelekeza kuhusu sisi wananchi wako. Achana na watamani madaraka.
 
Uzuri ni kuwa hakubaguliwa hata mmoja,na hata wengine waliamua kujiandalia mazingira ya kuondoka,ila mitazamo yao na matendo yao wanayafahamu wenyewe, wanataka nini, Mimi bado sifahamu, watuambie wenyewe.
 
Samia, Rais, wangu - nilikushangaa sana ulivyoanza kuwapa nafasi muhimu watu ambao wanajulikana kabisa kuwa nia yao ni kushika Urais. Hakuna asiyejua nchi hii mtu kama Mwigulu alipania sana kuwa contestant wa URais kwa mwaka 2025 na sasa haamini kama kufikia 2030 umaarufu wake utakuwa ni uleule. Hivi SSH ni kweli kabisa unaamini Dr. Mwigulu alifaa kushika hiyo nafasi? Kweli kabisa uliamini hivyo!
Mama SSH usipuuze ushauri huu, kuna majitu yanautaka huu uraisi kwa gharama zote huku yakijua wazi hayafai kuwa hata DC.
Kuwa makini na hawa watu kwani lengo ni kukuangusha huku unajiona!

Mtu kama huyu waziri wako wa 'kibubu' aliyoyafanya akiwa mambo ya 'nyumbani' ni aibu na dhambi kubwa sana mbele ya Mungu na hafai kabisa!
 
Wewe umeletwa kwetu na Mungu Mwenyewe wala sio na JPM, CCM au wapinzani. Ni Mwenyezi Munhu mwenyewe kakuleta sikiliza Mwenyezi Mungu anavyokuelekeza kuhusu sisi wananchi wako. Achana na watamani madaraka.
Huu ni ukweli usiopingika kwani hata 'sukuma gang' wanatakiwa kulijua hilo.
 
Uzuri ni kuwa hakubaguliwa hata mmoja,na hata wengine waliamua kujiandalia mazingira ya kuondoka,ila mitazamo yao na matendo yao wanayafahamu wenyewe, wanataka nini, Mimi bado sifahamu, watuambie wenyewe.
Kama sijakuelewa vizuri hapa!
 
Samia alichoshindwa kuelewa ni kuwa pamoja na kuwa alikuwa ni Makamu wa Rais hakuumbwa kuwaza au kufikiri au kutenda au kunena au kufanya kitu chochote kama alivyokuwa Mtangulizi wake.

Kwanza namna alivyowekwa pale na majukumu ya Makamu yalivyo KiKatiba alikuwa ni mtu passive tu - yaani kuangalia tu kilichokuwa kikitendwa na JPM bila yeye kuingilia au kufanya chochote.

Kwanza haikutegemewa kamwe kama Mwenyezi Mungu angeleta uamuzi ule na hivyo hakuna aliyewahi kufikiri kuwa Samia atakuja kuwa Rais wa nchi hii. Aliyekuwa anajua hilo ni Mwenyezi Mungu pekee

Samia, Rais, wangu - nilikushangaa sana ulivyoanza kuwapa nafasi muhimu watu ambao wanajulikana kabisa kuwa nia yao ni kushika Urais. Hakuna asiyejua nchi hii mtu kama Mwigulu alipania sana kuwa contestant wa URais kwa mwaka 2025 na sasa haamini kama kufikia 2030 umaarufu wake utakuwa ni uleule. Hivi SSH ni kweli kabisa unaamini Dr. Mwigulu alifaa kushika hiyo nafasi? Kweli kabisa uliamini hivyo!

Waziri wa Fedha hata awamu zilizopita alikuwa anachukuliwa mtu ambaye hakuonekana kamwe kuwa na dalili za kutaka uongozi wa juu wa nchi. Hapa Dr. Mwigulu hakuwa nafaa kabisa kwa sababu Waziri wa Fedha hapaswi kuwa mtu wa kubadilika badilika. Mf. mdogo ni Dr. Mpangao, huyu bwana pamoja na kuwa katika Serikali ya Jiwe lakini alikuwa ni mtu wa kusimamia zile principles za kifedha na hakuweka siasa nyingi sana kwenye hilo na ndiyo maana alidumu na isitoshe hamna hata mtu alimfikiria kuwa atakuja kuwa Makamu wa Rais. Kwa Mpango mama ulipiga bingo sana hata watu wengi kama walimtaka Majaliwa.

Sasa kwa huyu Mwigulu kigeugeu kwa hakika hutakaa usifiwe au upongezwe kama uliweka Waziri wa Fedha makini. Huyu mtu ni kinyonga huyu. Anabadilika na hana msimamo wake - anapenda kwenda na upepo na anatategemea wataalamu ambao wamebeba agenda za kisiasa.

Yeye mwenyewe hana msimamo wake unaoeleweka kwenye principles za uchumi. Kama anazo hebu tuambieni ni zipi? Dr Mpango tangu akiwa World Bank na hata Tume ya Mipango amekuwa akionekana kabisa ni mtu wa kutamani kukuza uchumi wa watu duni.

Hata kataika regime ya JPM pamoja na kujenga mamiundombnu lakini Mpango mara zote alikuwa akiongelea theories za kuinua wanyonge! Dr. Mwigulu huyu mwenye Phd ya juzi juzi tu na isiyoeleweka vizuri mnataka kutuambia principles zake hasa ni zipi?

Leo hii hata ukiamua kumweka Dr. Kimei kuwa Waziri wa Fedha waTanzania tutajua kabisa huyo Waziri atatupeleka kwenye kujenga uchumi kwa kupitia principles gani? Ukimchukua hata Prof. Mkenda yule Waziri wa Kilimo utaona kabisa anaweza kujipambanua kwa principles gani za uchumi

Hivi mama Samia ni vigezo vipi vilikufanya umchukue Dr. Mwigulu ambaye hakukaa sana kwenye Unaibu wa Wizara ya Fedha kuwa Waziri wa Fedha?

Huyu bwana alifanya kazi Benki Kuu kama Afisa tu wa kawaida na alikuwa Mwanaharakati kweli kweli na hakuwa hata mtendaji mzuri leo hii eti mnamfanya Waziri wa Fedha.

Huyu mtu hafai na asikupime Mhe. Rais wetu mwambie tu kisirisiri ajiuzulu ili huko baadaye umpe nafasi ingine! Akigoma kufanya hivyo TUMBUA una wengi wanafaa nafasi yake.

Hapo nimemsema Dr. Mwigulu tu lakini una mawaziri wengi tu ambao hawakufaa kwenda na wewe! Mungu kakutofautisha na wengine so unapaswa kufikiri kwa kadri Mwenyezi Mungu anavyokuongoza.

Wewe umeletwa kwetu na Mungu Mwenyewe wala sio na JPM, CCM au wapinzani. Ni Mwenyezi Munhu mwenyewe kakuleta sikiliza Mwenyezi Mungu anavyokuelekeza kuhusu sisi wananchi wako. Achana na watamani madaraka.
JPM keshaondoka hadi lini mtaendelea kumtajataja? Mnamiss kinoma bila shaka
 
Mawazo ya kipumbavu kabisa haya!

Basi hata yeye mwenyewe na selikali yake yote hawafai na hawana huruma maana nae akikuwa makamu wa rais!
Mbona hasira ndugu yangu Cremia ya Urusi,kwani umepewa pilipili pasi na hiari yako?tulia tuambie kakuudhi nani?
 
Katika mambo huyo mama alibugi ni kubaki na kundi kubwa la wale viongozi wa dhalimu. Maana hata kama ingekuwa kinyume chake bado dhalimu asingekubali kubaki na viongozi wa mtangulizi wake. Kama huyo mama anataka kubaki salama, apige chini mawaziri wote aliowaokota kwa dhalimu aanze na safu yake.
 
Angebakiza theluthi au robo tu ya Mawaziri ambao walikuwa kipindi cha JPM. Hapa alivyofanya atapata shida sana!
 
baraza zima la marehemu Pombe linapaswa kupigwa chini upesi.
No. Angebakiza wachache tu kwa ajili ya institutional memory. Kuwabakiza wote wanakuwa na nguvu kuliko hata yeye sasa. Wanaharibu mnooo! Wanajifanya wanataka kuupiga mwingi lakini wanshtukia wamebutua hapo hapo miguuni.
 
Back
Top Bottom