- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Hello JamiiCheck,
Nimeona mtandaoni ukurasa wa Mtandao wa X wa Watetezi TV ukikanusha madai ya kuwahi huchapisha taarifa ya Rais Samia akisema kuna madini kwenye baadhi ya hifadhi zetu na yanapaswa kuanza kuchimbwa kwakuwa Simba na Tembo hawali Madini.
Wao wanasema akaunti iliyoposti ni bandia, siyo yao lakini nakumbuka kama niliwahi kuiona mtandaoni siku za nyuma. JamiiCheck fanyieni uhakiki hili suala.
Nimeona mtandaoni ukurasa wa Mtandao wa X wa Watetezi TV ukikanusha madai ya kuwahi huchapisha taarifa ya Rais Samia akisema kuna madini kwenye baadhi ya hifadhi zetu na yanapaswa kuanza kuchimbwa kwakuwa Simba na Tembo hawali Madini.
Wao wanasema akaunti iliyoposti ni bandia, siyo yao lakini nakumbuka kama niliwahi kuiona mtandaoni siku za nyuma. JamiiCheck fanyieni uhakiki hili suala.
- Tunachokijua
- Julai 19, 2024, Uongozi wa kituo cha televisheni cha Mtandaoni cha Watetezi TV umewajulisha wafuatiliaji wake na umma kwa ujumla kuwa kumejitokeza ukurasa bandia katika mtandao wa kijamii wa X unaotumia jina lao la Watetezi TV kwa kupakia maudhui tofauti na kwamba watu wanapaswa kuacha kuufuatilia badala yake wafuatilie kurasa rasmi za Watetezi TV kwenye Mitandao yao ya kijamii ili kupata habari sahihi na za uhakika wakati wote.
Ukurasa huo unaodaiwa kutokumilikiwa na Watetezi TV pamoja na mambo mengine, umedaiwa kuchapisha taarifa inayomnukuu Rais Samia akisema "Kuna madini kwenye baadhi ya hifadhi zetu,Kule Serengeti na kwingine kuna aina za madini zimegundulika. Lakini TANAPA waligoma kabisa yasichimbwe ili kutunza uhifadhi. Lakini nataka sasa yachimbwe. Simba na tembo hawali madini."
Picha ya kanusho la Watetezi TV (Chanzo: Mtandao wa X)Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Baada ya kusambaa kwa taarifa hii pamoja na kutolewa kwa kanusho na Watetezi TV, JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hii ilichapishwa na Ukurasa wa Mtandao wa X wa Watetezi TV, Aprili 6, 2021. (Link imehifadhiwa hapa).
Utafutaji wa kimtandao ulifanywa na JamiiCheck kwenye Mtandao wa X kwa kutumia maneno "Kuna madini kwenye baadhi ya hifadhi zetu" umeleta majibu ya moja kwa moja yanayohusianisha chapisho hilo na ukurasa halisi wa Watetezi TV kama inavyooneshwa kwenye picha hapa chini.
Hadi Julai 19, 2024, saa 10:30 Jioni, Chapisho halisi lilikuwa bado lipo Mtandaoni kwenye ukurasa huo huo uliotumika kulikanusha. Uthibitisho upo hapa.
Akaunti ghushi zenye majina ya Watetezi TV
Katika hatua nyingine ya uhakiki, JamiiCheck ilikagua kuona ikiwa upo uwezekano wa kuwepo kwa Akaunti nyingine kwenye Mtandao wa X zenye majina ya Watetezi TV zinazopotosha taarifa kama inavyodaiwa.
Katika ufuatiliaji huu, imebainika uwepo wa akaunti mbili pekee zenye majina ya Watetezi TV kwenye Mtandao wa X kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini. Pia, mojawapo ya akaunti hizo iliyoandikwa kwa usahihi ni ile iliyotumika kuchapisha andiko tajwa Aprili 6, 2021 ambayo wakati huo ilikuwa haijathibitishwa (Kuwa na tick ya Bluu)
Picha yenye Akaunti zinazotumia jina la Watetezi TV kwenye Mtandao wa X
Kwa ufuatiliaji huu, JamiiCheck imejiridhisha kuwa Andiko hilo lilichapishwa na Akaunti rasmi ya Watetezi TV, Aprili 6, 2021, (kusoma uzi wa tamko la Rais Samia kuuza madini yaliyopo kwenye hifadhi angali hapa) siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwaapisha Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali aliokuwa amewateua, Ikulu Dar es Salaam. Hotuba ya uapisho huo imehifadhiwa hapa. (Kuanzia 1:42:35)
Pamoja na mambo mengine, Rais Samia alinukuliwa alisema anajua kuna madini katika maeneo ya TANAPA na Madini mengine ni muhimu hivyo alihoji tunayaweka pale ya nini wakati Simba na Tembo hawayali.
Sehemu nyingine ya hotuba ya Rais iliyofupishwa inayohusianishwa na chapisho la Watetezi TV imehifadhiwa hapa.