Watengenezaji wa maji ya Kilimanjaro acheni kuyachakachua, mnaua brand yenu

Themann

JF-Expert Member
Apr 15, 2022
3,842
16,044
Ni nani mwekezaji kwenye hii kampuni ya Kilimanjaro wakuu maana anauwa soko lake bila yeye kutambua miaka ya nyuma kidogo hii kampuni maji yake mtu wa kawaida ukinywa basi.

Unajiweza lakini sijui Nini kimewakuta maji yao ni machachu hafadhali maji ya kisima au Bomba.

Yani nakunywa maji yao si mara ya kwanza Wala ya pili naona kitu kile kile na mikoa tofauti au maji yao yana classes kwamba kwenye conference kubwa kubwa wanawekewa Yenye ubora?

Wahusika acheni kuchakachua mnaua brand Yenu.

Ni ushauri tu kwenu.

PXL_20230625_151532652.jpg
 
kwa sasa yana chumvi yanazidiwa hata na afya ama hill mkuu sijui wamekuja kuwaje afu lita moja 500 kwa sasa
Nadhani tangu mengi Atutoke kampuni imeporomoka muwekezaji aliopo saivi amekubali kampuni Bora liende tu Yani ni hafadhali unywe kandoro kuliko hayo maji saivi.
 
Nadhani kuna dawa za kuuwa wadudu WA maji zitakua updated ndo sababu ladha imebadilika , Wanapokea malalamiko kwenye kopo kuna address zao
Nitanunua Tena then niwape malalamiko sasa kwanini na bei washushe zamani 1l iliuzwa 1500 saiv 500
 
Ntayajaribu mkuu japo dar yapo maduka machache
Ni kweli mkuu, yawezekana wao hawajui lakini hayana tena ule ubora kama wa awali.
Labda yanachakachuliwa somewhere on the way?
Au mtaalam wa PH alishaondoka?
Kwa sasa tunajaribu sana kuyakwepa kwa kweli
 
Ni nani mwekezaji kwenye hii kampuni ya Kilimanjaro wakuu maana anauwa soko lake bila yeye kutambua miaka ya nyuma kidogo hii kampuni maji yake mtu wa kawaida ukinywa basi.

Unajiweza lakini sijui Nini kimewakuta maji yao ni machachu hafadhali maji ya kisima au Bomba.

Yani nakunywa maji yao si mara ya kwanza Wala ya pili naona kitu kile kile na mikoa tofauti au maji yao yana classes kwamba kwenye conference kubwa kubwa wanawekewa Yenye ubora?

Wahusika acheni kuchakachua mnaua brand Yenu.

Ni ushauri tu kwenu.

View attachment 2668652
Mbona hii brand ishakufa longtime! Mpaka wamepunguza bei lakini wapi
 
Ni kweli mkuu, yawezekana wao hawajui lakini hayana tena ule ubora kama wa awali.
Labda yanachakachuliwa somewhere on the way?
Au mtaalam wa PH alishaondoka?
Kwa sasa tunajaribu sana kuyakwepa kwa kweli
Yani wamepitwa hata na afya.
 
Ni kweli mkuu, yawezekana wao hawajui lakini hayana tena ule ubora kama wa awali.
Labda yanachakachuliwa somewhere on the way?
Au mtaalam wa PH alishaondoka?
Kwa sasa tunajaribu sana kuyakwepa kwa kweli
PH iko vile vile 7.0. Sema wamejaza madini na michumvi (Sodium) kibao...🚮🚮🚮

Sasa hivi ni mwendo wa Dew Drop, Buyegi, Hill na Afya tu.
 
Back
Top Bottom