Watendaji wa mtaa walindwe na kuthaminiwa

boni200

Member
Jul 21, 2017
16
6
Nimekua nikifuatilia sana majukumu ya watendaji wa kata na mtaa hasa wa mtaa wana changamoto kubwa sana hasa waliopo Dar es salaam.

Sikatai kuna wengine hawana maadili lakini wengi wanakumbana na changamoto sana hasa kwenye kazi zao.

Leo nitazungumza kuhusu mauziano ya ardhi hapa Kuna ulazima wa serikali kubadili na kuja na Sheria mpya ambayo itawalinda hawa watendaji wa mtaa ambao mwisho wa siku wanaangukia kubaya tena na kuishia gerezani kwa makosa ambayo miundo ya utendaji wao ingekua sawa wasingefika hatua ya kua gerezani.

Nitakuja na kisa kimoja cha mtendaji mmoja amabae mwaka 2021 akiwa katika mkutano mmoja huko halmashauri alipigiwa Simu na wajumbe wake kuhusu mauziano ya ardhi kati ya jamaa aliyefahamika kwa jina maarufu sana kama dalali, na watu wengine kadhaa na mnunuzi alikua ni mtu mmoja mzito anafanya kazi idara ya serikali.

Muuzaji aliyefahamika kwa jina hilo na mnunuzi (wote jina kapuni) Walikuja ofisi ya serikali ya mtaa huo wakiombwa kisainiwa mauziano Yao ambayo mtendaji na baadhi ya wajumbe ambao sio wa eneo ambalo ardhi ipo inafanyika walikuepo, mnunuzi alioomba sana mauziano yafanyike baada ya hapo wale waliokuepo ofisini kwa siku Ile waliwapigia Simu mtendaji na Mwenyekiti mtendaji akasema kama eneo halina shida bhasi wasaidieni.

Siku chache badae ikagundulika eneo lile lililouzwa muuzaji sio mmiliki ni baada ya huyo bibi mmoja kujitokeza. Sintofahamu ikaja bibi akiambiwa hati hana lakini yule muuzaji wa pili akaonyesha hati amabyo mnunuzi wa pili nae alionyesha na ndie hadi alihusika kutengeneza akaunti ya benki kwa huyo muuzaji.

Sasa baada ya tukio hilo mtendaji alishikiliwa na kushtakiwa tena kwa kesi ya uhujumu uchumi na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, huku madalali wakiwa nje hawajakamatwa na wakati huo mjumbe wa eneo alithibitisha kwa mtendaji wake ni kweli eneo hilo mmiliki ni huyo muuzaji wa pili na huyo bibi hajawahi kumuona?

Ombi langu watendaji wa mtaa wote nchini epukeni kupokea aina yeyote ya zawadi ambayo baada ya mauziano ya ardhi kufanyika mnapewa kama kifuta jasho acheni wao wenyewe wagawane pesa zao ridhikeni na hicho.

Pili serikali iangalie namna nzuri ya kuweza kubadili muundo ikiwezekana Kila eneo au kata kuwepo na afisa Ardhi.

Tatu serikali iandae na kuweka electronic system data base ambayo itawafikia watendaji wote wa mtaa katika kuhakiki maeneo yanayouzwa au ardhi inayouzwa ili kama Kuna eneo halieleweki bhasi mauziano yasitishwe.

Watendaji nao ni watu wanapaswa kuheshimiwa Mtindo unaoitwa Chezo Dar es salaam umewaathiri watendaji wengi na kuharibu utu wao pia madalali ndio chanzo kikubwa.

Tutumie Saini za watendaji vizuri
 
Back
Top Bottom