Watatu mikononi mwa polisi kwa uvamizi mkutano wa CUF

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
92,421
112,075

Watatu mikononi mwa polisi kwa uvamizi mkutano wa CUF

Kwa ufupi
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatatu) Sirro amesema shauri la kesi hiyo limekwishafunguliwa na upelelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika huku akitoa rai kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotoa vitisho kuwa watawafuata watu fulani ili kuwashughulikia.

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amesema mapaka sasa watu watatu wanashikiliwa kuhusiana na tukio la kuvamiwa kwa mkutano wa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatatu) Sirro amesema shauri la kesi hiyo limekwishafunguliwa na upelelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika huku akitoa rai kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotoa vitisho kuwa watawafuata watu fulani ili kuwashughulikia.

“Hakuna mtu au kikundi cha watu wanaweza kuwa na mamlaka ya kuwashambulia wenzake mtu kama ana malalamiko yake anapaswa kuyapeleka mahakamani na kama ni ya jinai ayapeleke polisi lakini sio kuwavamia watu kama vile wewe upo juu ya sheria,”amesema Sirro.

Chanzo: Mwananchi
 
Kipande kimewageukia CUF - Maalim. Kamanda amewabana wenye mkutano,kwa nini wamemkata mapanga,kumwumiza kiasi kile mlinzi wa Prof,kuna justification yoyote kwa kipigo kile, hakuna aliye juu ya sheria. CUF maalim wametumia nguvu kubwa pasipo uhalali
 
Huyo nae anayejidai kupendwa na wanawake usiku,hana maana yoyote,ni kada, mtumwa na Mlinda ccm mkuu.maigizo yake sio kua yamechosha tu,yanatapisha.huyo mtu anatia aibu majeshi ya polisi duniani.huko sio kutumika tena, nizaidi ya kutumika,na niaibu.eti "mikononi mwa polisi "! ,mikono ya polisi inafanana hivyo ? Awatume yeye na kumlinda lipumbavu amlinde,alafu awatie mikononi tena ! Yeye ni muajiriwa wa ccm asitukejeli sisi.
 
Kipande kimewageukia CUF - Maalim. Kamanda amewabana wenye mkutano,kwa nini wamemkata mapanga,kumwumiza kiasi kile mlinzi wa Prof,kuna justification yoyote kwa kipigo kile, hakuna aliye juu ya sheria. CUF maalim wametumia nguvu kubwa pasipo uhalali
Ile inaitwa self defence.. Suala la msingi umewavamia wao wamejihami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…