Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 336
- 866
Nchi kwetu Tanzania katika kipindi hichi cha miaka hii 2, taifa litakuwa bize kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika November 27, 2024. Na uchaguzi mkuu ambao utafanyika 2025.
Katika kipindi hiki wanasiasa wameshaanda sukari zao za hoja kuja kudanganya au kusema ukweli wakati wakujinadi kwenye kampeni katika chaguzi zote mbili. Ambapo baadhi ya wananchi wengine wanaweza kuingia kwenye mtego kama siku zote na wengine kushutukiaa mchezo huo.
Naamini kila mmoja anauwezo wa kutafakari na kupima mambo au jambo kwamba hili ni sahihi au si sahihi. Mimi niseme na wananchi wezangu ambao watashindwa kuzitambua kodi za wanasiasa waongo na wanakuja kwenye majukwaa kwaajili ya maslai yao binafsi.
Kwanza kila uwezavyo fika kwenye kampeni zao sikiliza hoja anazotoa na pima kwa miaka mingine iliyopita je kuwa hiyo hoja inaweza kutekelezeka na kiongozi huyo. Mfano mdogo kuna sera mgombea atakuwa anajinadi nazo lakini kiuhalisia unaona kabisa hapa na pigwa changa la macho tu.
Sikiliza vipaumbele vyake vitakavyokuwa muhimu zaidi kwa kila mwananchi yoyote yule.
Usibaguwe kampeni za wagombea wa vyama hivyo vya siasa. Wewe ukipata nafasi udhuria kampeni zote wa vyama vyote vya kisiasa ambapo utapata uhalisia wa yupi umpe kura yako.
Usikubali kupokea rushwa ya aina yoyote hile. Hapa ndipo patamu na wananchi wengi wanapotezwa na upepo wa rushwa kwa kupewa vitu mbalimbali kutoka kwa wanasiasa wenye nia chafu na dhuluma tu. Utaona wanatoa jezi kwa vijana kwaajili ya mpira , wengine watatoa kanga, kofia, t shirt n.k. Sasa mwananchi mwezangu kama wewe ni mzalendo na nchi yako na unataka mabadiliko basi kaaa mbali na Rushwa yoyote hile kwenye kipindi hiki cha uchaguzi.
Hata wengine wataanza kutembea nyumba kwa nyumba na kufanya vikao vyao na baadhi ya wananchi kwa kuwapamba na vijisenti kwenye bahasha za kaki. Usikubali kabisa maana utakuwa unajiteka mwenyewe.
Cha mwisho Nenda kajiandikishe ili uwe na haki ya kupiga kura maana usipojiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura utakuwa umejikatili wewe mwenyewe na kizazi chako.
Soma Pia: