Watanzania wengi hawataelewa hii kitu kwa miaka mingi ijayo

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
3,186
8,624
KWA HISANI YA MARTIN MARANJA MASESE (MMM)

UFAFANUZI WA (The Political Service Retirement Benefits Act [CAP. 225])

Wanufaika wa Sasa: -
. Mke wa Mwl, Julius K. Nyerere, Maria Nyerere.
• Wake wa Ali H. Mwinyi, Sitti na Khadija Mwinyi.
• Mke wa Benjamin W. Mkapa, Anna Mkapa
• Mke wa Jakaya M. Kikwete, Salma Kikwete
• Mke wa John P. Magufuli, Janeth Magufuli
• Mume wa Samia S. Hassan, Hafidh Ameir

Kwa mujibu wa The Political Service Retirement Benefits Act [CAP. 225] kila mwezi wenzi hawa watalipwa 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

Kama Rais aliyepo madarakani anapokea TZS 50,000,000 kwa mwezi, mwenza wa Rais atalipwa malipo/mafao ya TZS 30,000,000 kila mwezi.

Rais akistaafu, mwenza/wenza wake atapokea/watapokea (kwa mkupuo) 25% ya mshahara wa Rais alioupokea wakati wote akiwa madarakani.

Mfano, kama Rais alikaa madarakani kwa kipindi cha miaka 10, akalipwa TZS 4,000,000,000, mwenza wake atalipwa TZS 1,000,000,000 kwa mkupuo.

Pamoja na malipo hayo ya fedha, pia wenza hawa sita (6) wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapata mafao mengine kama ilivyoelekezwa;

Nyumba ambayo Rais alipewa na alikuwa akiitumia kama makazi baada ya kustaafu itakuwa mali yake halali baada ya mume/mke wake (Rais) kufariki.

2. Atapokea posho ya matengenezo ya kila mwezi katika maisha yake yote akiwa hai kiasi ambacho ni sawa na 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani.

3. Mke/mume wa Rais atatibiwa ndani na nje ya Tanzania, na matibabu yake yatagharamiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

4. Mjane wa Rais mstaafu atapata huduma ya magari mawili, na dereva wawili kufanya shughuli zake za kila siku. Serikali inalipia gharama za mafuta.

Magari anayopewa mjane wa Rais yatabadilishwa baada ya miaka 5. Kuna maintenance allowance. 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani kila mwezi

6. Malipo ya fedha kulipa mishahara kwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara ya watumishi kwa; dereva, mpishi, mfua nguo na mtunza bustani

7. Mke/mume wa Rais atapata huduma ya usafiri kwa gharama za serikali hadi mahali pa kuishi kwa maisha yake yote hadi pale ambapo kifo kitawatenganisha.

8. Mke/mume na watoto wanapata ulinzi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Usalama wa Taifa.

9. Gharama za mazishi ya mke/mume wa Rais yatakuwa chini ya serikali. Serikali ya Tanzania itagharamia kwa 100% msiba wa mwenza wa Rais

10. Mjane wa Makamu wa Rais, anapata stahiki kama za mjane wa Rais isipokuwa tofauti yake ni moja, atapata gari moja la Serikali na dereva mmoja.
 
Duh
But this is not fair at all!
 
Haya mabadiliko ya hovyo na aliyeanzisha ni salma kikwete .
Kama samia hajausaini hayo mabadiliko ni vyema akayakata.
Hivi inakubalikaje mbunge kupeleka hoja bungeni inayomgusa yeye binafsi diretcly yaani moja kwa moja.
Hivi wabunge nao si wanaweza wakaibua hoja na wenza wao oia walipwe mafao .
 
Huu ujinga ulishapingwa sana
Na aliyeanzisha hoja hii na Salma Kikwete Mbunge na pia Mkee wa Rais Mstaaf Jakaya Kikwete.
Inakuaja mbunge akaanzisha hoja bungeni kumuhusu yeye binafsi.
Hawa wake wa viongozi wao ni special sana au. wanakuwa kwenye maisha magumu waume zao wakifa ?
Kwa kweli dhumuni kuu la huu mswada ni ulafi uliopitiliza na ubinafsi wa hali ya juu wa Salma Kikwete .

 
Aisee
 
..vipi kuhusu viongozi wenye wenza zaidi ya mmoja?

..pia yuko kiongozi mmoja alikuwa mkorofi wa kuoa, na kuacha, wakati yuko madarakani.
 
Hii sheria ni ya hovyo sana.
Nchi kama Kenya vijana wangeingia road.
Ila kwa sisi aaaaagh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…