Watanzania wanaweza kuiga wakenya kuieleza ukweli huu wa bajeti ya Kenya ya 2024/25

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
819
867
Wakuu, nimekuta ripoti ya gazeti la thestandard la kenya toleo la leo kuhusu maoni ya wananchi baada ya bajeti hiyo kupendekeza mambo kadhaa hasa ongezeko la.kodi.

Wiki ijayo Mwigulu Nchemba, ambaye aliwahi kudokeza kuongeza tozo, atawasilisha bajeti ya serikali ya 2024/2025.

Wananchi wa Kenya wamekuja juu baada ya serikali kupanga kuondoa ruzuku ya mkate na maziwa, kuongeza ushuru wa magari nk.

Jumuiya ya waislamu ya Kenya imewataka wanachi kuacha kuwachagua wabunge ambao watawaunga mkono bajeti hiyo inayokwenda kuwaathiri wananchi ambao tayari wana hali ngumu.

imesema serikali inafuja fedha za umma kwa matumizi yasiyofaa hasa safari za ndani na nje ambapo kwa kipindi cha miezi tisa iliyopita imetumia shilingi bilioni 18.18 za Kenya

Imesema badala ya rais kusafiri kila mara akiambatana na watu wengi, angeitumia wizara ya mambo ya nje ili kupunguza gharama.

Jumuiya hiyo pia imeeleza kuwa ongezeko la deni la nje unapalekea matumizi makubwa ya fedha, lakini matumizi ya mikopo hiyo hayaonekani.

Aidha wafanyabiashara wadogo wamesema Rais Ruto amekiuka ahadi yake wakati wa uchaguzi ya kupunguza bei za bidhaa na sasa zinaongezeka.

Tutegemee hali tofauti kwa bajeti ya Mwigulu? Watanzania wataipokeaje?

 
Back
Top Bottom