Huwezi kumtumbua mtu aliyekataa mshahara ukaacha aliyesababisha vifo kwa mamia ya watanzania! Yaani unawalisha watu unga wa mihogo unawaambia kua ni dawa! hii ni dhambi mbaya sana.Hii inaonyesha ni jinsi gani nchi inaendeshwa kisanii
Haki ipo mbinguni...hapa sana sana atapewa adhabu ya kumwagilia maji bustani ya hospitali.
Halafu hiyo familia ni kasheshe tupu,mama ndio mwanzilishi wa hayo mambo ya sijui Deci sijui upatu,watu wali lizwa sio mchezo miaka ile na haikuwapo kesi wala nini, ni watafutaji wasiojali matokeo ila kama desturi chama kina wanusuru.Sisiemu madabidaaa daresalaaam. Kulindana kama kawa, jipu gumu alitumbuliki kama LUGUMI meeeen
Njia ni moja mkuu hupitia mahospitalini, Ispokua hua zinalipiwa na wafadhili moja kwa moja, Sasa kama wewe ni mzalishaji unapokea hayo mabilioni ya afadhili.Hapa pesa za wajanja waliziona ndo wakafungua kiwanda wakasaga unga wa mihogo wakapaki kama dawa pesa zikapigwa. Zakawa packed kama ARVs Wagonjwa wetu wakanywa wakifikiri na ARVs. Huu inawezekana ni mtandao mkubwa hata waganga wa mikoa watakua wanajua vizuri.Wanasema dawa za arvs hospital wanagawa bure inamaana hizo dawa feki yeye alikua anamuuzia nani?
Hilo ni moja tu la kutisha na lina target specific group of people in our society.Hivi kweli jamani mtu anatengeza ARVs fake, anasambaza kwa maelfu ya Wanzania wanaoishi na VVU wanakunywa wakidhani ni dawa za kuwaongezea maisha! Is this serious? Hivi tunaelewa kasi ya ongezeko Virusi kwa mwili wa mwathirika asiyetumia dawa? Ni Watanzania Wangapi wamepoteza maisha kwa kutumia kutumia hizo ARVs zilizothibitika kua ni fake?
Hivi hili suala lingetokea kwenye nchi kama ya China au kwa majirani pale Rwanda hawa watu wangeendelea kuranda mitaani kweli? tena wengine viongozi?
Inaumiza inaumiza inaumiza mno. Hata kama Rais atumbue majipu lakini moja lakini hayawezi kufanana na haya majipu ya ARVs fake kamwe.
Sijui hii kesi imefikia wapi mpaka sasa, Sidhani kama kuna watu wameguswa na hili na kuumia zaidi ya wale ndugu waliopoteza ndugu zao kwa matumizi ya ARVS fake.
Hivi huyu mtanzania aliyeenda akakaa na kufikiria kutengeneza ARVs fake alifikiria nini? Huyu mtu anaamini kwamba kuna Mungu kweli? Anatengeneza unga sijui ni wa mihogo au mahindi akiaminisha watu kua ARVS kweli?
Kwakweli vyombo vyetu vya dola juu ya hili kuona wahusika wamatembea mitaani haviwatendei haki Watanzania.